MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja
Bi.Ghanima Sheha akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Mkoa huo,huko katika Ukumbi
wa Mkoa wa Mjini ulioopo Amani Unguja.
|
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini kabla ya kukabidhi Vifaa. |
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini
Mhe.Faharia Khamis Shomari (kulia),akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la
Magomeni Ndugu Khadija Rajab Pazi (kushoto).
|
|
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari(kulia) akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Malindi Ndugu Salma Said Muumin. |
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini
Mhe.Faharia Khamis Shomari akimkabidhi Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Ndugu Asha
Mzee Kiti Kimoja na Meza Moja vya Ofisi.
|
KATIBU wa UWT Mkoa wa Mjini Ndugu Stamili akitoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali ya Kiutendaji katika Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa huo kilichofanyika sambamba na kukabidhi Vifaa kwa Akina Mama. |
MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Mhe.Saada Ramadhan,akizungumza katika hafla hiyo. |
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini
Mhe.Faharia Khamis Shomari,amekabidhi Vifaa mbali mbali vyenye Thamani ya
Shilingi Milioni 15 kwa Majimbo yote ya UWT ndani ya Mkoa huo.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti 451,Meza
Moja ya Ofisi na Mashine Moja ya kutengenezea Chaki ikiwa ni sehemu ya
kuunga Mkoa juhudi za Ujasiliamali za Akina Mama wa Mkoa huo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Vifaa
hivyo Mbunge huyo Mhe.Faharia amesema lengo la kutoa Vifaa hivyo ni kutekeleza
Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020.
Mhe.Faharia ameeleza kuwa Akina Mama wa UWT
ndani ya Mkoa huo pamoja na majukumu ya kisiasa waliyokuwa nayo bado wanatakiwa
kujiajiri wenyewe kupitia ujasiriamali hivyo vifaa vilivyotolewa vitawasaidia
katika harakati hizo za kujiajiri wenyewe.
Pamoja na hayo alitoa Wito kwa Wanawake wa
rika mbali mbali ndani ya Mkoa wa Mjini kushiriki kaiunga Mkoa CCM ili ishinde
katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.
Katika hafla hiyo Wawakilishi wa Viti Maalum
wa Mkoa huo ambao ni Mhe.Mgeni Hassan Juma ameahidi kutoa Mashine mbili za
Photocopy kwa UWT Wilaya ya Amani na Mjini huku Mhe.Saada Ramadhan amekabidhi
Mifuko Mitano ya Jipusamu kwa ajili ya kutengenezea chaki na kuahidi shilingi
Milioni Moja kwa kila Wilaya zilizomo katika Mkoa huo.
Wakizungumza kwa wakati tofauti Makatibu wa
UWT wa Majimbo yote yaliyomo katika Mkoa huo, wameahidi Vifaa hivyo kuvitunza
na kuhakikisha wanavitumia katika matumizi yaliyokusudiwa.
Awali akifungua Kikao cha Baraza Kuu la UWT
Mkoa wa Mjini Mwenyekiti wa Mkoa huo Ndugu Ghanima Sheha,amesema Kikao hicho
kitajadili masuala mbali mbali ya kiutendaji na kutoa maelekezo ya kiutendaji
juu ya ufanikishaji wa majukumu mbali mbali ya UWT na CCM kwa ujumla.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni