VIJANA wa matembezi ya kuenzi waasisi wa Mapinduzi wakiwa na Picha za Marais wa Sasa wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano pamoja na Marais wastaafu ambao ndio waasisi wa Mapinduzi hayo. |
BAADHI ya vijana wakiwa na bango lenye ujumbe unaoeleza maudhui ya matembezi hayo |
VIJANA wapiganaji wa UVCCM wakiwa katika matembezi hayo huku wakionyesha utimamu na ukakamavu walionao katika kulinda na kutetea Mapinduzi ya mwaka 1964. |
MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheri James akitoa salamu za UVCCM Tanzania nzima katika kuenzi Mapinduzi. |
MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita akiwasalimia vijana wa UVCCM katika Mapokezi ya Matembezi hayo yaliyofanyika katika kiwanja cha Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui. |
VIJANA wa UVCCM wakiwa katika matembezi hayo. |
BAADHI ya Viongozi wa UVCCM na Serikali ya SMZ walioshiriki matembezi hayo. |
VIJANA wa UVCCM wakiwa katika matembezi hayo huku wengine wakitiwa moyo kwa kufarikijiwa licha ya kuchoka kwa masafa na uchovu wa kutembea umbali mrefu. |
BAADHI ya Wenyeviti wa Mikoa mbali mbali ya UVCCM Zanzibar wakiwa katika matembezi hayo. |
BAADHI ya vijana na Wajumbe wa NEC walioshiriki matembezi hayo. |
VIONGOZI mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi walioshiriki katika matembezi ya UVCCM |
VIJANA mbali mbali wa UVCCM walioshiriki katika matembezi hayo wakiwa katika kijiji cha Mwera kabla ya kuanza matembezi hayo. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla Mabodi akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi katika mapokezi ya matembezi ya UVCCM ya kuwaenzi waasisi wa Mapinduzi. |
KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Abdulghafari Idrissa Juma akizungumza katika mapokezi ya UVCCM. |
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali idd akihutubia vijana zaidi ya 1000 walioshiriki matembezi hayo kutoka Mikoa yote ya Zanzibar na Tanzania bara. |
MSOMA Qur'an tukufu Ostadh Shaaban Mohamed Abdallah akisoma Aya zinazoendana na malengo ya matembezi hayo |
VIJANA wa Brass Bandi ya UVCCM wakionyesha uhodari wao katika matembezi hayo |
WASANII wa ngoma ya Asili ya kibati kutoka Zanzibar wakitoa burudani katika matembezi hayo. |
KIKUNDI Cha wasanii kutoka Kisiwani Pemba wakitoa burudani ya wimbo maalum wa Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla Mabodi akiwa na baadhi ya vijana wa UVCCM kutoka Tanzania bara walioshiriki katika matembezi hayo. (PICHA NA ABEID MACHANO NA IS-HAKA OMAR) |
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi ameeleza kuwa Taifa linawategemea Vijana kusimamia kwa vitendo Mapinduzi ya kuondoa vitendo viovu vinavyoikabili nchi ikiwemo Rushwa, ufisadi, Dawa za Kulevya na udhalilishaji wa Kijinsia.
Alisema vitendo hivyo visipondoshwa sasa ni hatari kwa ustawi wa maendeleo ya Taifa kwani vinatia doa juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali zote mbili chini ya usimamizi wa Chama cha Mapinduzi.
Pia alibainisha kuwa Taifa kupitia Serikali zote mbili inahitaji kuona Vijana wake wanakuwa chemchem ya kustawisha Maendeleo badala ya kuwa dimbwi la vurugu na migogoro isiyokuwa ya lazima.
Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alisema hayo wakati akiyapokea Matembezi ya Vijana 1,000 wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hapo katika Viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Alisema Mapinduzi yametekelezwa na Wazalendo wa Visiwa vya Zanzibar kwa lengo la kuondoa matendo mabaya ikiwemo ufisadi, uzembe, uonevu ubaguzi wa aina zote zile pamoja na mambo yote yanayorejesha nyuma au kukwamisha juhudi za kujiletea maendeleo.
Balozi Seif alisema Dhama hiyo ya Mapinduzi Daima ya Marehemu Mzee Abeid Aman Karume ya kuondoa mabaya na kuleta mambo mema warithi wake wa halali ni Vijana ambao Serikali ina wajibu wa kuwajengea mazingira bora ikiwemo suala la ajira litakalowawezesha kuwa na utulivu wa kutekeleza jukumu walilokabidhiwa na Taifa.
Alisema serikali inaendelea kuchukua hataa stahiki ya kupunguza changamoto za ukosefu wa ajira kwa Vijana hapa Nchini kwani ushahidi uko wazi wa nafasi moja ya ajira kugombaniwa na zaidi ya Vijana 20.
Alisema miongoni mwa juhudi za Serikali katika kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa Vijana ni kuongeza nafasi za mafunzo ya amali nchini ambapo tayari vituo Viwili vya mafunzo hayo vinajengwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja na Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alieleza Vituo hivyo vitafanya idadi ya Vituo Vinne vya amali nchini ambavyo vinategemewa kuchukuwa idadi kubwa ya Vijana ambao watakapomaliza mafunzo yao watakuwa na uwezo wa kujiajiri wao wenyewe badala ya kusubiri ajiza za Serikalia mabzo kwa kipindi hichi bado finyu.
Balozi Seif alieleza mpango mwengine wa uhakika wa kupambana na changamoto hiyo ni ule wa kukuza Uchumi kwa njia ya kukaribisha Wawekezaji katika sekta ya Utalii itakayokuwa na uwezo mkubwa wa kubeba Vijana wengi.
Alieleza Mrdi mkubwa kuliko wote uliowekezwa Afrika Mashariki wa Zanzibar Amber Resort wenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 1.6 sawa na shilingi za Kitanzania Trilioni 2.1 unategemewa mkombozi kwa Vijana wengi Visiwani Zanzibar.
Balozi Seif amewapongeza Vijana wa Uzalendo wao wa kulitumikia Taifa la Tanzania kwa moyo thabiti bila ya kuweka mbele maslahi ya fedha badala yake wawe na uzalendo usioyumba wa kulinda nchi.
Akizungumzia matakwa ya vijana wa CCM ya kushauri kuifuta Serikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK) yanayotokana na CUF kususia uchaguzi wa marudio uliopita, Balozi Seif alisema hilo ni suala la Kikatiba ambalo wananchi wenyewe hasa wa CCM watalibariki kwa kupatikana viti vingi katika Baraza la Wawakilishi kupitia Uchaguzi Mkuu ujao ili kupata nguvu za kuondosha mfumo huo ndani ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Aliongeza kuwa uondoaji wa Suala hilo unahitaji uwepo wa kura ya Maoni itakayotoa ridhaa ya Wananchi mfumo upi wanauhitaji kuufuata.
Akitoa salamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Nd. Kheri James alisema katika kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 na asiyejua wala kuthamini umuhimu wake anastahiki kuwajibishwa.
Kheri alitahadharisha wazi kwamba Mtu au kikundi kinachojitokeza kuchezea shere Mapinduzi ya Zanzibar awe makini kupata dhoruba za Vijana wa Chama cha Mapinduzi chenye asili ya Mapinduzi hayo.
Alisema ili Mapinduzi yaendelee kuwa na Heshima lazima Jamii iyalinde na kuyatetea kupitia Vijana watakaokuwa tayari kujitolea muhanga kwa kulinda heshima hiyo ya Taifa.
Naye Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Tabia Maulid Mwita amesema vijana wa Chama Cha Mapinduzi wapo tayari kulinda mapinduzi ya mwaka 1964 kwa gharama yoyote bila ya kujali vikwazo na sera hoja dhaifu zinazojengwa na vyaa vya upinzani nchini.
Amewasihi vijana wa UVCCM kuendelea kuwa imara na wenye msimamo katika kulinda na kutetea maslahi ya Serikali zote mbili ya Zanzibar pamoja na ya Jamguri ya Muungano wa Tanzania huku wakitamba na kujivunia kuwa miongoni mwa vijana wazalendo waliolelewa katika malezi bora ya kisiasa na kijamii ndani ya Chama cha Mapinduzi.
“ Nashindwa kuelezea furaha niliyonayo kutoka moyoni kwa kupata fursa hii ya kujumuika na vijana wenzangu pamoja na Wazee na Macomrade wa zamani wa UVCCM kujumuika nao katika matembezi haya”, ameeleza Tabia.
Akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho anayefanyia kazi zake Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla (Mabodi) amesema matembezi hayo sio tu kwamba yaenzi waasisi wa Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964, bali yanawakilisha ujasiri,msimamo na dhamira ya vijana wa sasa katika kulinda historia halisi ya mapinduzi isifutike katika Anga za kimataifa na kitaifa.
Akizungumzia msimamo wa CCM kuwa ni kuhakikisha dhana ya mapinduzi inakuwa ni ngao ya kusimamia sera za maendeleo endelevu kwa wananchi wote bila ya ubaguzi wa rangi, kabila na kidini.
Amesema Maendeleo yaliyopatikana chini ya usimamizi wa Serikali zote mbili chini ya usimamizi wa Rais Dk.Shein pamoja na Rais Dkt. Magufuli ni kielelezo tosha cha kuieleza Dunia kwamba Tanzania inaongozwa na Chama cha Mapinduzi(CCM) Kinachojali maisha na utu wa watu wote na sio uchu wa madaraka wa kuwanufaisha watu wachache.
“Wananchi nikuelezeni kuwa CCM ipo imara na itaendelea kuchapa kazi na kusimamia kikamilifu Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 ili wananchi wanufaike na matunda ya Mapinduzi hata wale wanaotupinga na kubeza maendeleo ya nchi yetu tulioshindana nao toka enzi za ASP wakiwa ni Hizbu na sasa ni Chama cha CUF nao wataendele kunufaika”, ameeleza Dkt. Mabodi na kufafanua kuwa maendeleo hayana Chama na hata wapinzani wameanza kuelewa taratibu huku wakijiunga na CCM kwa wingi.
Mapema Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Nd. Abdulghafar Idrissa alisema Vijana wa Umoja huo wameridhika na utekelezaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wote.
Alisema Jamii inaendelea kushuhudia miradi mbali mbali mikubwa na midogo inayoibuliwa na Serikali katika pembe zote za Visiwa vya Zanzibar ikilenga kustawisha maisha ya Wananchi wote bila ya ubaguzi.
Hata hivyo Kaimu Naibu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM Zanzibar alielezea masikitiko yake kutokana na baadhi ya Watendaji wa Serikali ngazi za kati wenye tabia ya kuwasengenya na kuwanyanya Vijana wa CCM wakati wanapohitaji huduma katika Taasisi wanazozisimamia.
Alitoa onyo kwa watendaji hao ambao wote wanaeleweka kuacha tabia hiyo kwani dawa yao yao ya kuwatangaza hadhani itatangazwa ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni