Jumatatu, 8 Januari 2018

BALOZI SEIF KUPOKEA MATEMBEZI YA UVCCM JANUARI 9,MWAKA HUU.

 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa  Balozi Seif Ali Idd.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, anatarajiwa kupokea matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Januri 9 mwaka huu katika ofisi kuu ya CCM Kisiwandui.

Akizungumza na Zanzibar Leo ofisini kwake Gymkana, Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Abdul-ghafar Idirisa Juma, alisema matembezi hayo yataanzia kijiji alikozaliwa muasisi wa mapinduzi, marehemu Abeid Amani Karume, Mwera Kiongoni wilaya ya kati Unguja.

Alisema matembezi hayo yataanza saa 12:00 asubuhi na kuongozwa na Mwenyekiti wa umoja huo, Kheri Jemes.

Alisema lengo la matembezi hayo ni kuendelea  kuyaenzi mapinduzi ya 1964 ambayo yanatimia miaka 54 Januari 12, 2018.

Hivyo aliwaomba vijana watakaoweza kushiriki matembezi hayo kuthibitisha ushiri wao kwa Katibu wa umoja huo kwenye wilaya zao.

Kauli mbinu ya matembezi hayo ‘maendeleo ya Zanzibar ni matunda ya mapinduzi yetu"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni