Jumamosi, 20 Januari 2018

MATUKIO KATIKA PICHA KHITMA NA DUA YA AROBAINI YA KUWAOMBEA ASKARI 10 WA JWTZ WALIOUWAWA DRC KONGO


 MSIKITI wa Noor Muhammad(SAW) ambao ndio ulisomwa Khitma na Dua ya kuwaombea Askari wa JWTZ waliouwawa hivi karibuni nchini DRC Kongo walipokuwa wakilinda Amani, na Khitma hiyo imeandaliwa na Kamati ya Amani Kitaifa Zanzibar.

 BAADHI ya waumini wa Dini ya Kiislam wakiingia katika Msikitini kwa Ajili ya kushiriki Khitma hiyo.

 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Dk.Hussein Mwinyi (kulia)  mara baada ya kuwasili katika msikiti huo kwa ajili ya shughuli ya Khitma.

 BAADHI ya viongozi mbali mbali wa dini na serikali wakiwa katika shughuli hiyo ya Khitma na Dua.
 VIONGOZI wa SMT, SMZ  na wawakilishi wa Majeshi ya UN akiwemo ( Wa pili kushoto ni Meja Jenerali Sharif Sheikh Othman, ambaye ni Kamanda wa Brigedi ya Nyuki (101KV) Zanzibar.
 NAIBU katibu Mkuu wa CCM  Zanzibar  Dk.Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' (wa pili kutoka kushoto aliyevaa miwani na koti nyeusi).
 BANGO la ujumbe Maalum wa Khitma hiyo ulioandaliwa na Kamati ya Amani Kitaifa Zanzibar.



NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk.Mabodi na viongozi wengine wakiwa katika kisomo.
 MJUMBE wa Kamati ya Amani Kitaifa Alhaji Mussa Salim kutoka Dar es saalam akitoa mawaidha katika shughuli hiyo ya Khitma.

 WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Dk.Hussein Mwinyi akitoa tamko la shukrani juu ya maandalizi ya kongamano hilo kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jonh Pombe Magufuli.

 MWENYEKITI wa Kamati ya Amani Kitaifa Sheikh Salim Mohamed AL-Kadil akisema machache na kumkaribisha mgenu rasmi.

 KATIBU wa shughuli Sheikh Said Mayugwa akitoa neno la shukrani kwa wananchi na ndugu wa marehemu walioudhuria Khitma hiyo. 
 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni Mlezi wa Kamati ya Amani Kitaifa akihutubia katika Khitma hiyo.


 BAADHI ya viongozi, wananchi, wageni mbali mbali walioudhuria Khitma hiyo wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi.

 KATIBU wa Shughuli hiyo, Sheikh Said Mayugwa akisoa shukrani kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya Khitma hiyo.

 MAOSTADH  maarufu kama Mapacha wa Mtume(SAW) Hussein Nassor na Hassan Nassor kutoka Dar es saalam wakiimba Kaswida yenye maudhui yanayoendana na Khitma hiyo 

 PICHA ya pamoja ya  Balozi Seif  na viongozi mbali mbali wa Kamati ya Amani, wageni waalikwa wa SMZ na SMT.

 KATIBU Mkuu wa Kamati ya Amani Kitaifa Sheik Fadhil Soraga akizungumza na TBC mara baada ya kumalizikika Khitma hiyo.(PICHA NA IS-HA OMAR)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni