MWANASIASA Mkongwe visiwani Zanzibar ambaye pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama cha Afro-Shiraz Party iliyoungana na TANU ikazaliwa CCM, Ndugu Baraka Mohamed Shamte.
MWANASIASA Mkongwe visiwani humu Baraka Shamte amesema
Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad hana
jipya na kwamba anachotakiwa kukifanya
wakati huu ni kuwapotosha Watanzania juu ya mustakabali wa uhai wa Chama chake.
Amesema Katibu Mkuu huyo amemalizwa kisiasa na Mwenyekiti
wake Profesa Ibrahim Lipumba hivyo ni ishara tosha kuwa anamuogopa hivyo anachopaswa kukielezea muafaka wao
umefikia wapi kati yao.
Akizungumza Shamte amesema
kuwa siku za hivi karibuni Maalim Seif aliitisha mkutano na waandishi wa habari
na kuelezea kuwa viongozi wanapaswa
kuwasikiliza viongozi wa dini wakati kwa upande wake ndani ya chama chake hasikilizi ushauri wa
mtu.
"Maneno haya ni ya kisiasa kabisa angekuwa anasema haya ndani
ya Chama chake anasikiliza ushauri tungemuona wa maana lakini hataki ushauri alafu unaongea maneno
hayo hiyo ni ishara kuwa siasa imeanza kumtupa mkono,"amesema.
Shamte ameongeza kuwa Katibu Mkuu huyo mara nyingi
ameambiwa achie uongozi kutokana na
kuchokwa kwake lakini kila anayemwambia anafukuzwa unachama ndani ya chama chake
hakuna demokrasia ya kweli badala yake anajifanya mfalme.
Amesema mwanasiasa huyo ndani ya chama chake hataki
kuambiwa ukweli ambapo ametaja mfano
kuwa baadhi ya wanachama wake
walimshauri ashiriki kwenye uchaguzi wa marudio wa mwaka 20 lakini alikataa
na kuwafukuza watu hao. Katika maelezo yake Shamte amefafanua kuwa Katibu huyo
hataki ushauri ndani ya chama chake wala kusikiliza la kuambiwa badala yake anawasikiliza wafadhili wake kutoka baadhi ya nchi zinazounga mkono mfumo wa
siasa za Kiliberali.
"Maalim Seif amechoka kisiasa hana tena jipya yeye
anazua mambo ambayo watanzania hawataki
kuyasikia na kwamba wanataka kufahamu mustakabali
wa chama chake watu wanajiuliza hali yake na
Profesa Lipumba iko je kwa sasa, kuna kipindi fulani Aboubakar ambaye ni mwanachama wa CUF alichukua fomu katika
mkutano mkuu wa kujaza fomu ya kugombea nafasi ya Katibu, Seif alikataa na alitaka agombee pekee
yake,"amefafanua Shamte.
Mwanasiasa huyo ameeleza kuwa ndani ya CUF hakuna demokrasia badala ya kuzungumza mustakabali wa chama
chake anasema mambo ya uongo hiyo ni dalili kuwa siasa sasa basi tena kwake.
"katika mkutano mkuu huo ambao ulifanyika Bwawani
Seif alijitangaza mshindi kabla ya kutangazwa
na chama chake hivyo akitaka kuzungumza siku
nyingine mambo hayo ya kuwa viongozi wasikilize
viongozi wenzao aanze yeye kusikiliza viongozi
wenzake ndani ya chama chake,"amesema Shamte.
Ameongeza kuwa Maalim Seif asitake kuwadanganya watu kwa kuzungumza
mambo yasio kuwa na maana na kwamba Watanzania watambue kuwa Profesa Lipumba ametwaa ubingwa wa kisiasa ndani
ya CUF hali inayopelekea Maalim Seif kukosa ajenda za kuwambia wafuasi wake.
Shamte ambaye kisiasa ni mwalimu wa walimu anayestahiki
kupewa heshima ya kuwa Profesa wa siasa
na historia, ameeleza kwamba kutokana na migogoro iliyokomaa ndani ya CUF Maalim Seif anatakiwa kuachia madaraka kwa
viongozi Vijana yasije kumkuta kama
yaliyotokea Zimbabwe enzi za mwisho za Rais mstaafu wa nchi hiyo Robert
Mgabe.
“ Siasa za zama hizi Maalim Seif haziwezi tena tayari afya
yake kimwili na kiakili zimechoka japokuwa kiumri kwangu ni mdogo sasa lakini
kawa mzee na kuzeeka kifikra kutokana na kukumbatia visasi,chuki na siasa za kuwachonganisha wananchi
badala ya kuwaunganisha”,, amesema Shamte na kumshauri mwasiasa huyo
ajiweke kando na siasa kutokana na kukosa sifa za kuwatumikia wafuasi wa Chama
chake.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni