KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka(kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Abdulghafari Idrissa Juma wakiwa Ikulu Zanzibar kwa ajili ya utambulisho wa viongozi wakuu wa Jumuiya hiyo.
NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR.
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ulioongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri D. James akiambatana na Makamu Mwenyekiti UVCCM Ndugu Tabia M. Mwita pamoja na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Ndugu Shaka H. Shaka na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Abdulhafar Idrissa Juma wamekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo Jumanne Januari 16, 2018 Ikulu mjini Zanzibar.
Uonhozi wa UVCCM alionyesha hisia na furaha kwa namna ambavyo Dk. Ali Mohamed Shein anavyoendelea kujali, kuthamini, kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya Wananchi.
“Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini Rais Dk Ali Mohamed Shein imeendelea kujali, kuthamini na kushughulikia shida , kero na matatizo ya wananchi hatimaye kuyapatia ufumbuzi stahili . UVCCM tumeridhishwa mno na kasi ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015/2020” alisema Kheri.
Mwenyekiti Kheir alitumia nafasi hiyo pia kuwaasa Vijana kuwa na desturi ya kwenda kuchota busara na hekima toka kwa Wazee wetu ili kuweza kukomaa kisiasa.
“Vijana mnapokwenda kwa Wazee kiuhalisia mnakwenda kuchota busara na hekima. Vijana bila ya msukumo wa fikara na mawazo ya wazee , hatuwezi kujifunza jambo lolote na kukomaa kisiasa .UVCCM Tumeridhika na utendaji wa SMZ katika mkakati wa kuzitazama shida na maisha ya Wananchi.” alisema Kheri.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni