Jumamosi, 13 Januari 2018

UZALENDO USITUTOKE WANACCM

Mhe. Thuwaiba E. Kisasi akizungumza wanachama wa UWT huko Dunga
NA EMMANUEL MOHAMED, ZANZIBAR

MAKAMU Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi(UWT),Thuwayba Kisasi,amekabidhi kadi kwa wanachama wapya 250 ambao wamejiunga na chama,wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini.

Akiwapokea wanachama hao katika ukumbi wa shule ya Msingi ya Dunga, ambapo ni sehemu ya ziara yake ya katika kuimarisha jumuiya hiyo ya UWT ndani ya mkoa huo ambapo aliwasisitizia kuzingatia maadili ndani ya chama na kwamba wanapaswa kuyaheshimu.

Thuwayaba alisema UWT inapaswa kuunganisha nguvu ili kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa mwaka 2020 na kwamba jambo ambalo ni la muhimu zaidi ni kuwa wazalendo ndani ya chama pamoja na jumuiya hiyo.

"Kunatakiwa kuwepo na maadili na uzalendo katika serikali ambayo inaongozwa na chama chetu pamoja na ndani ya chama na itikadi za CCM ni kuwa uzalendo usitutoke somo la uzalendo na urai yana umuhimu sana wakati wetu tulipokuwa tunasoma tulikuwa tunafahamu kuwa hii ni nchi yetu na hichi ni chama chetu kwa hiyo unakuwa mzalendo ndani ya chama na serikali ikilinganishwa na sasa," alisema.

Makamu huyo aliongeza kuwa kwa kuwa kunatarajiwa kuwepo na mafunzo maalum katika mkoa huo ambao utawahusisha viongozi wapya wa UWT ndani ambao wamechaguliwa katika uchaguzi wa hivi karibuni ndani ya chama hivyo ni wajibu wakapatia masomo ya uzalendo na uraia.

Alisema mafunzo hayo yatawasaidia kuwapatia kufahamu wapi taifa lilipotoka na historia halisi ya chama na mwelekeo wake pamoja na jumuiya hiyo ya UWT na jambo hilo litawawezesha chama kusonga kwa pamoja.

"Tunawajibu wa kulinda nchi yetu na ninawapongeza kwa kuingia ndani ya chama hivyo ni wajibu wetu kupinga hali ya fitina na kusema ukweli daima na kuilinda taifa letu,"alisema 

Aliwataka wanachama hao wapya kuhakikisha wanayafuata na kuyazingatia maadili na si kuyasema mdomoni tu bali kwa vitendo ikiwemo kuheshimu itikadi ya chama cha CCM.

Mbali na hilo, Makamu Mwenyekiti huyo aliwakumbusha wanajumuiya hao kulipa ada za kadi zao na kwamba kulimbikiza madeni ya muda mrefu si vizuri hususan katika kipindi cha mabadiliko ya CCM mpya ambapo inatarajiwa kuanza kutumika kadi za kietroniki.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa UWT, Zanzibar, Salama Aboud alisema UWT ya sasa iko imara baada ya viongozi waliochaguliwa kuwa madhubuti hivyo inatarajiwa kuwa ni miongoni mwa jumuiya za chama ambazo zitaleta ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Aliwakumbusha wanajumuiya hiyo kuanza kulipa ada zao ili kuisadia chama na UWT katika kuraisisha kuendesha shughuli za kila siku za jumuiya hiyo.

"Kuna changamoto kubwa ndani ya jumuiya hii katika mkoa huo kuwa omba omba kutokana na kutokuwepo kwa miradi ambayo itaweza kusaidia kujiendesha yenyewe hivyo ni wakati sasa ya kuanza kusimama yenyewe,"alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoa huo, Shemsa Abdallah alimuahkikishia Makamu Mwenyekiti huyo kuwa UWT ndani ya mkoa huo itaendelea kuwa imara wakati wote na kutatua changamotoz zilizoko kwa kubuni miradi ambayo itasaidia kujiendesha yenyewe.

Alisema UWT mkoa huo imejipanga kuhakikisha inafanya kazi kwa muda wote ili kuleta ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa mwaka 2020 kuanzia ngazi za udiwani, wabunge,wawakilishi hadi nafasi za urais.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni