Jumapili, 19 Agosti 2018

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA DK.BASHIRU PEMBA.

 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akivishwa sikafu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Pemba akitoka Unguja. 
KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mwl.Kombo Hassan Juma mara baada ya kuwasili Pemba kwa ajili ya kuendelea na ziara yake kisiwani humo.

 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake Suleiman Sarahan mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili ya ziara ya kujitambulisha. 

 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Tabia Maulid Mwita mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Pemba.

 KATIBU Mkuu wa CCM Dk,Bashiru akiangalia  ngoma ya kirumbizi kutoka Mkoa wa kusini Pemba ambayo ni miongoni mwa mapokezi ya kiongozi huyo.

 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru akipokelewa na vijana wa UVCCM kwa wimbo wa mashujaa katika Uwanja wa Ndege wa Pemba.

 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally na msafara wake wakitembea  kwa maandamano ya mapokezi kuelekea ofisi ndogo ya CCM Chake chake mjini Pemba.


Mwenyekiti wa  Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Pemba  Ali Hamad Khatib  akimpokea na kumpa nasaha Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru baada ya kufika katika Ofisi Ndogo ya CCM Pemba.


 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania  Dk.Bashiru akizungumza na Watumishi wa CCM wa Ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.

 MWANACHAMA mpya kutoka CUF Amina Juma Kassim  ambaye ni miongoni mwa wanachama waliohama katika chama hicho na kujiunga na CCM, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally.


 
 BAADHI ya Wana-CCM wakifuatilia kwa karibu matukio yanayoendelea katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru uliofanyika leo katika Ukumbi wa skuli ya Fidel Castro.

 KATIBU Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akiwahutubia wanachama na viongozi wa CCM katika ukumbi wa skuli ya Fidel Castro Mkoa wa Kusini Pemba.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru katika ukumbi wa Skuli ya Fidel Castro.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa  wa Kaskazini Pemba  Ndugu Mbwerwa Hamadi Mberwa akimkabidhi zawadi ya ndizi ya mkono wa Tembo Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru  Ally katika ziara ya kujitambulisha kwa wanachama wa CCM Pemba.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndugu Mbwerwa Hamad Mberwa  ya ngao ya mwenge wa uhuru Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru kutoka Mikoa miwili ya Pemba.


 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba Yussuf Ali Juma akiwakaribisha viongozi mbalimbali katika Mkoa wa Kusini Kichama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni