Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Dk.Bashiru Ally akiwapungia mkono viongozi mbali mbali wa CCM waliokuwa uwanja wa ndege kwa ajili ya kumuaga na kumsindikiza baada ya kumaliza ziara yake na kuelekea Dar es saalam kwa ajili ya majukumu yake.
NA IS-HAKA OMAR,
ZANZIBAR.
KATIBU Mkuu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Dk.Bashiru Ally amesema Chama hicho kinadhibiti ubadhilifu wa mali na matumizi mabaya ya rasilimali fedha ili kijitegemee
kiuchumi.
Amesema endapo rasilimali hizo zitatumika
vizuri na kuanzishwa kwa miradi mingine mikubwa ya uzalishaji wa kipato katika
ngazi mbali mbali za chama na jumuiya ili ziwanufaishe wanachama wote badala ya
watu wachache.
Kauli hiyo katika ziara yake kisiwani Pemba wakati akizungumza na
viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wa Mikoa Miwili katika ukumbi wa
Fidel Castro uliopo, Mkoa wa Kusini Pemba.
Dk.Bashiru ameeleza
kuwa lengo la kusimamia dhana ya ukuaji wa uchumi ndani ya chama kupitia vyanzo
vyake vya mali na fedha ni kukiondosha chama katika mazoea ya kutegemea
ufadhili wa watu wenye fedha wanaokuwa na malengo ya kujinufaisha wenyewe
kisiasa.
Pia ameyataja malengo
mengine kuwa ni uimarishaji wa maslahi ya watumishi wa CCM na jumuiya zake
kwani bado maslahi yao ni ya kiwango cha chini ambayo hayaendani na hadhi ya
taasisi yenyewe.
Ameeleza kuwa malengo
hayo yakifanikiwa utakuwa ni ushindi mkubwa kwa wanachama wa CCM wote kwani
tabia za rushwa na makundi ya kusaka nafasi za uongozi kwa kutumia fedha
yatakuwa yamedhibitiwa.
Amewasisitiza
viongozi wote wa taasisi hiyo kuunga mkono malengo hayo kwa kuhakikisha
wanapunguza matumizi holela ya fedha na badala yake waanzishe miradi
itakayowasaidia kujiendesha ili kulinda heshima na hadhi ya CCM mbele ya jamii.
Pamoja na hayo
amezitaka taka jumuiya zote hasa ya umoja wa vijana (UVCCM) kuhakikisha
wanakuwa wabunifu kwa kutumia rasilimia walizonazo kwa kuanzisha miradi mikubwa
ya kilimo, uvuvi na viwanda vidogo vidogo ili vijana wajiajiri wenyewe.
Katibu Mkuu huyo
Dk.Bashiru amewaka wazi msimamo wa Chama
Cha Mapinduzi kuwa wale wote waliohusika na kutapeli na kujimilikisha mali za
taasisi hiyo kinyume na utaratibu wote watachukuliwa hatua za kisheria.
Naye Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi alisema wanachama wote wana haki ya
kuunga mkono mambo mema yanayotekelezwa na taasisi hiyo kwa nia ya kuongeza
ufanisi.
Amesema wakati wa
vyama vya ukombozi vya ASP na TANU viongozi wa wakati huo walifanikiwa kupanga
mambo ya maendeleo yaliyodumu kwa muda mrefu kutokana na umoja na mshikamano
waliokuwa nao hasa katika masuala ya kuvijenga kimaendeleo vyama vyao.
Dk. Mabodi ameeleza kuwa suala la uzalendo katika kusimamia
maslahi ya kitaifa ni jambo muhimu hasa kwa viongozi wanaoaminiwa na kupewa
dhamana za kuongoza jamii.
Akizungumzia ushindi
wa CCM visiwani Zanzibar mwaka 2020 alisema mpaka sasa Zanzibar hakuna upinzani
bali kuna vikundi vidogo vidogo vya watu wanaojivisha joho la upinzani wakati
wao ni madalali wa kisiasa waliofilisika kifikra.
Naibu Katibu Mkuu
huyo amesema CCM itashinda kisayansi kutokana
na serikali zake kutekeleza mahitaji ya wananchi wa mijini na vijijini kupitia
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni