Alhamisi, 16 Agosti 2018

DK. BASHIRU AWASILI ZANZIBAR.


  KATIBU Mkuu Dk.Bashiru Ally(kulia) akisalimiana na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao (kushoto), mara baada ya kuwasili Zanzibar.

 KATIBU Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally (kushoto) na Naibu  Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla (Mabodi) pamoja na viongozi mbali mbali walioshiriki katika mapokezi hayo wakiimba nyimbo mbali mbali za Chama Cha Mapinduzi wakielelea katika Chumba cha VIP kwa ajili ya mazungumzo mafupi.
 
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla (Mabodi) akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume akitokea Dar es saalam leo.

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

VIONGOZI na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla (Mabodi), wamempokea Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally aliyewasili visiwani humo kwa ajili ya kuanza ziara yake ya mwanzo ya kikazi na kujitambulisha katika Mikoa sita ya Kichama Zanzibar.

Dk.Bashiru amewasili jioni ya leo kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Aman Karume na kupokelewa kwa shangwe na vifijo na wanachama,viongozi na makada mbali mbali wa CCM.

Katika Mapokezi hayo Dk. Mabodi ameambatana na Makatibu wote wa Idara za CCM Zanzibar, wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa pamoja na viongozi mbali mbali kutoka Wilaya na Mikoa sita ya CCM na Jumuiya zake.

Ujio wa Katibu Mkuu huyo ni kwa ajili ya ziara yake inayotarajiwa kuanza kesho tarehe 17/8/2018 kwa upande wa Unguja na kuhitimisha ziara hiyo tarehe 20/8/2018 kisiwani Pemba.

Katika ziara yake hiyo Dk.Bashiru atazungumza na viongozi mbali mbali wa Chama na Jumuiya zake pamoja na vikundi mbali mbali vya vijana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kwa Mikoa yote ya Kichama.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni