Jumapili, 12 Agosti 2018

MATUKIO KATIKA PICHA BONANZA LA MICHEZO KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA DUNIANI.

 WAZIRI wa Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali  Abeid Karume akifungua bonanza la Michezo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani.
 VIONGOZI mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi, SMZ na taasisi binafsi walioshiriki katika bonanza la michezo wakiimba wimbo maalum katika bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya ZSSF Uhuru Park Kariakoo Unguja.


 VIJANA wa kikundi cha sarakasi cha Bungi Bihole Acorobatic wakionyesha uwezo wao katika bonanza hilo.


 KIKUNDI Cha Sarakasi kutoka Wilaya ya Magharibi ''B'' wakionyesha ujuzi wao katika boanza  hilo la michezo.

 VIJANA wadogo wawili ambao ni miongoni mwa washiriki wa vikundi vya sarakasi vilivyoshiriki katika maonyesho hayo wakiwa katika picha ya pamoja kato ya Mkuu wa Mkoa wa Mjiini  Magharibi , Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud , Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Dk.Abdullah Hasnuu Makame wakiwa katika picha ya pamoja na vijana hao.


 BAADHI ya vijana mbali mbali kutoka taasisi tofauti walioshiriki katika bonanza hilo wakifutilia michezo mbali mbali inayofanyika katika viwanja hivyo.

 WASANII wa mziki wa kizazi kipya wakionyesha ujuzi wao kupitia  bonanza hilo.

 WAZIRI wa Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Balozi Ali Aman Karume akicheza mchezo wa Pool Table katika mashindano ya mchezo huo katika bonanza la kilele cha maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa upande wa Zanzibar.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akikimbia mbio za kupokezana vijiti ikiwa ni moja ya mashindano ya bonanza la Michezo ambayo ni miongoni mwa kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani.

 VIJANA mbali mbali walioshiriki katika bonanza hilo wakishindana kuvuta kamba.

 VIONGOZI mbali mbali wa SMZ, CCM na UVCCM wakicheza mchezo wa keramu.

 WANANCHI walioshiriki katika bonaza hilo wakionyesha uwezo wao wa kucheza mchezo wa bao.

VIONGOZI kutoka taasisi mbali mbali wakishiriki katika mchezo wa kufukuza kuku.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni