Jumanne, 19 Februari 2019

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA DK.SHEIN WILAYA YA KATI UNGUJA TAREHE 19/02/2019.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiweka jiwe la Msingi Shule ya Maandalizi na Msingi ya Uzi Ng'ambwa leo katika mwendelezo wa ziara yake katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hawapo pichani)akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Uzi Ng'ambwa mara baada ya kuweka Jiwe la msingi katika shule ya msingi na maadalizi ya Kijiji hicho.

 WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa shule hiyo huko Uzi Ng'ambwa. 
 BAADHI ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika hafla hiyo.


 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akitoa salamu za CCM katika Mkutano wa Majumuisho ya ziara hiyo ya Wilaya ya Kati Unguja huko Hoteli ya Coconut iliyopo Marumbi.

 BAADHI ya Viongozi wa CCM na wananchi mbali mbali wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Hafla hiyo.

 WAZIRIN wa Nchi (OR) Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizowasilishwa katika Taarifa ya Chama na Serikali katika Mkutano wa Majumuisho ya Ziara.

 BAADHI ya Wananchi wakiwa katika hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwe la Msingi.

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Aboud Jumbe akitoa ufafanuzi wa mikakati ya Serikali kuimarisha miundombinu ya Barabara katika kiijiji cha Uzi Ng'ambwa.

  BAADHI ya Viongozi wa CCM na wananchi mbali mbali wakifuatilia hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika Hafla hiyo.

 MKURUGENZI Mkuu Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) ndugu Mussa Ramadhani Haji akitoa ufafanuzi juu ya juhudi za Serikali katika kutatua tatizio la upungufu wa Maji katika Kijiji Cha Uzi Ng'ambwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni