KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao akitoa kadi kwa mwanachama mpya huko Tawi la CCM Bambi. |
|
WANACHAMA wapya 10 waliopokea kwa niaba ya wenzao 93 wa CCM wakila kiapo cha uanachama mara baada ya kukabidhiwa kadi hizo. |
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao akiwahutubia wanachama wa CCM katika Tawi la CCM Bambi. |
KATIBU wa CCM Tawi la Bambi Said Hussrin Haji akisoma risala ya Tawi hilo. |
NA IS-HAKA
OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU wa Kamati
Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao
ameagiza uongozi wa Tawi la CCM Bambi Wilaya ya Kati Unguja kuanzisha Darasa la Itikadi kwa Vijana wa mbali mbali wa Tawi hilo.
Agizo hilo amelitoa
leo katika hafla ya kuwakabidhi kadi za CCM wanachama wapya 93 waliojiunga na
CCM kupitia Tawi hilo.
Amesema kila kijana
wa CCM anatakiwa kupikwa kiitikadi, kiuongozi na kisiasa katika madarasa ya
itikadi hivyo Tawi la Bambi na Matawi mengine ndani ya Mkoa wa Kusini Kichama
Unguja yasiyokuwa na madarasa hayo wayaanzishe.
Ameeleza kwamba
mwanachama mzalendo, mwadilifu na mchapakazi lazima apitie katika madarasa hayo
yanayotoa elimu ya siasa na historia halisi ya Zanzibar na Chama cha Mapinduzi
kwa ujumla.
Aidha ameeleza kuwa
Serikali ya Awamu ya Saba chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed
Shein imetekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa ufanisi mkubwa mijini na
vijini.
Katika maelezo yake
Katibu huyo, amesema miundombinu ya Barabara za viwango vya lami , umeme,afya,
elimu, maji safi na salama,kilimo, uvuvi vyote vimeimarika katika maeneo mbali
mbali ya mijini na vijijini.
Amesema CCM chini
ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John
Pombe Magufuli ameendelea kusimamia kwa vitendo siasa za maendeleo
zinazoelekeza Chama kufanya siasa na uchumi.
Aidha amewasisitiza
wanawake na vijana wa Bambi kuchangamkia fursa za ujariamali kwa kuanzisha
vikundi mbali mbali ili waweze kupewa mikopo yenye masharti nafuu kutoka
Serikalini na wajiajiri wenyewe.
Ndugu Catherine
amewakumbusha amewataka wanachama wapya kuhakikisha wanalipia kwa wakati kadi
zao pia wajifunze masuala mbali mbali kwa kusoma miongozo na kanuni za CCM.
Aidha amewambia
wanachama hao kuwa kwa sasa CCM ipo katika wiki ya maadhimisho ya Sherehe za
kuzaliwa kwake ambapo inatimiza miaka 42 toka kuasisiwa kwake kutoka katika
Vyama vya Ukombozi vya ASP na TANU.
Naye Mwenyekiti wa
Tawi hilo ndugu Silima Haji Vuai amesema bado wanaendelea na mikakati mbali
mbali ya kukiimarisha chama hicho ili
kulinda historia halisi ya Kijiji cha Bambi ambacho ni miongoni mwa mashina na
chimbuko la harakati za ukombozi wa Chama cha ASP.
Akisoma risala
Katibu wa Tawi hilo,Ndugu Said Hussein Haji amesema kijiji cha Bambi na maeneo
jirani wameimarika kisiasa na bado wanaendeleo kuongeza wanachama wapya ili
kwenda sambamba na maelekezo ya Chama.
Kupitia hafla hiyo
Chama Cha Mapinduzi kimevuna wanachama 93 na wamekabidhiwa kadi wanachama 10
kwa niaba ya wenzao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni