Jumanne, 12 Februari 2019

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA RAIS WA Z'BAR DK.ALI MOHAMED SHEIN LEO WILAYA YA MJINI UNGUJA.


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kuwasili katika Eneo la Mnara wa Mbao Kilimani Zanzibar kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi katika  Ujenzi wa Tangi kubwa la Maji Safi na Salama lenye uwezo wa kuchukua Lita milioni 1,000,000, katika ziara yake ya kukagua miradi mbali mbali ya Serikali Zanzibar iliyoanza leo Tarehe 12/02/2019.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akizindua rasmi Jiwe la Msingi la Tangi la Maji Safi na Salama linalojengwa Mnara wa Mbao Kilimani Zanzibar.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kulia) ,Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (wa kwanza kulia),Waziri wa Ardhi, Maji , Makaazi,Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe.Salama Aboud Talib (wa pili kushoto) wakipewa maelezo ya ujenzi wa Tangi hilo.

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndugu Catherine Peter Nao (kulia) akihojiwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Kutoka KISIWANDUI Ndugu Daud Ismail Juma (kushoto)  juu ya ziara hiyo ya kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 huko Saateni katika ujenzi wa Tengi la Maji Safi na Salama la Lita Milioni 2,000,000.

 WAKUU wa Idara mbali mbali za Chama Cha Mapinduzi CCM Zanzibar, wakiwa katika eneo la Saateni katika uwekaji wa Jiwe la msingi  wa Tangi la Maji Safi na Salama.


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akifungua Jiwe la Msingi Ujenzi wa Tenki la Maji Safi na Salama la Saateni katika Mwendelezo wa Ziara yake Wilaya ya Mjini Leo.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipewa maelezo ya michoro mbali mbali ya matenki ya Maji yanayojengwa eneo la Saateni na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA ndugu Mussa Ramadhan Haji.

 VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi wakiimba Wimbo wa Mashujaa wa SISI SOTE katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa Maji Saateni.




 Waziri wa Ardhi, Maji , Makaazi,Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe.Salama Aboud Talib akizungumza katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi Saateni.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akisisitiza namna Serikali inavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/2020.

 VIONGOZI na Wanachama mbali mbali wa CCM wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Amani Mkoa wakifuatilia hotuba ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara yake leo.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mjini Ndugu Talib Ali Talib akizungumza katika Mkutano huo.
 VIONGOZI mbali mbali wa CCM wakiwa katika Mkutano wa Chama Cha Mapinduzi ambao ni Sehemu ya ziara ya Dk.Ali Mohamed Shein.



  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wanachama,Viongozi na Watendaji mbali mbali wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja katika ziara yake leo.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza katika mkutano wa Dk.Shein na wanachama wa CCM.

VIONGOZI mbali mbali wa CCM wakiwa katika Mkutano wa Chama Cha Mapinduzi wakimsikiliza Dk.Shein.

 Mbunge wa Jimbo la Amani Mwalim Mussa Hassan akitoa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mara baada ya kuwahutubia wanachama wa Chama hicho.

PICHA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO CCM ZANZIBAR.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni