WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk. Sila Ubwa Mamboya akitoa ufafanuzi juu ya faida watakayoipata wananchi wa Wilaya ya Mkoani wanaotumia Barabara ya Mkanyageni-Kangani. |
KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe. Mustafa Aboud Jumbe akitoa maelezo ya kitaalamu juu ya ujenzi wa Barabara hiyo. |
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara Pemba. |
MAELFU ya Wana CCM na Wananchi mbali mbali walioudhuria katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Barabara ya Mkanyageni-Kangani Pemba.
(PICHA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO AFISI KUU CCM ZANZIBAR.)
NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amesema Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 imeeleza kwa ufasaha namna Serikali itakavyoimarisha miundombinu ya Barabara ili kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri.
Amesema katika kutekeleza azma hiyo Serikali inaendelea kuimarisha mitandao ya barabara yenye viwango vya lami mijini na vijijini kwa lengo la kwenda sambamba na matakwa ya miongozo ya CCM kupitia Ilani ya uchaguzi ya Taasisi hiyo.
CRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali
Mohamed Shein, amesema Serikali ina azma ya kujenga barabara mpya kutoka
Chakechake hadi Mkoani, kutokana na umuhimu uliopo na kukidhi mahitaji ya
wakati.
Ufafanuzi huo ameutoa mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Barabara ya Mkanyageni-Kangani(KM5) Wilaya ya Mkoani Pemba.
Dk. Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesema amewataka wananchi wa maeneo mbali mbali katika wilaya hiyo kuitunza barabara hizo ili zidumu kwa muda mrefu.
Katika maelezo yake Dk. Shein ameeleza kuwaSerikali ina azma ya kujenga barabara mpya kutoka
Chakechake hadi Mkoani, ili isaidie kurahisisha mitandao ya usafiri baina ya Wilaya hizo mbili ambazo ni kitovu cha biashara na shughuli za kijamii.
Amesema ujenzi wa barabara ya Mganyageni-Kangani uliainishwa katika Ilani ya mwanzo ya Uchaguzi wa mwaka 1965 ambapo Dk.Shein alikuwa ni mgombea uwakilishi kupitia jimbo hilo, na toka wakati huo serikali za awamu mbali mbali ziliandaa mazingira Rafiki ya kujenga barabara hizo kwa maslahi ya wananchi.
Aidha amesema Serikali ya SMZ kupitia CCM ilipoahidi kutenga barabara hizo wapo baadhi ya wananchi waliobeza ambao kwa sasa pia wananufaika na barabara hizo katika Maisha yao ya kila siku.
Dk.Shein amewasisitiza wananchi wa Wilaya hiyo kuacha kutumiwa na baadhi ya wanasiasa wanaopotosha kila jambo jema linalotekelezwa na Serikali.
Kupitia hotuba yake Dk.Shein amewasihi wananchi kuendeleza mshikamano na kuepuka migogoro isiyokuwa na manufaa kwa maendeleo ya wananchi wa Kisiwa cha Pemba.
Kupitia ziara ya Dk.Shein Kisiwani Pemba, endelea kufuatilia Matangazo ya moja kwa moja mbashara(Live) kupitia Bahari FM Radio na Ukurasa wa Facebook wa Ikulu Zanzibar.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni