CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
Zanzibar kimepokea kwa mshutuko,majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha
Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Bumbwini ndugu Ali Haji Pandu (70) aliyefariki
ghafla nyumbani kwake Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
Akizungumza Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ wakati akiifariji
familia ya marehemu huyo, amewaomba ndugu,jamaa na marafiki wa karibu wa
marehemu kuwa na subira katika kipindi hichi cha msiba huo.
Dk.Mabodi amesema kuwa
Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuthamini juhudi za uchapakazi,uzalendo,uongozi
bora na weledi wa marehemu Ali Haji enzi za uhai wake alikuwa ni kiongozi na
muumini wa kweli wa kuimarisha maendeleo ya taasisi hiyo.
Amesema taasisi hiyo
imepoteza kiongozi shujaa aliyepigania maslahi ya CCM kwa vitendo na aliweza
kusimamia mipango endelevu ya ushindi wa CCM katika jimbo alilolioongoza.
Katika maelezo yake
Dk.Mabodi amesema kwa sasa jambo la pekee la kumsaidia marehemu huyo ni
Vuongozi,Wanachama, Watendaji na Wananchi kwa ujumla kumuombea Dua Marehemu ili
aweze kupokelewa katika makaazi mema peponi amin.
Naibu Katibu Mkuu huyo wa
CCM Dk.Mabodi alifuatana na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja
chini ya Mwenyekiti wa Mkoa huo ndugu Idd Ali Ame.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni