Jumamosi, 2 Februari 2019

MHE.ANGELINA: ATOA MILIONI 3.5 ,ATAKA WANAOWACHAFUA VIONGOZI WAPUUZWE.


 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Angelina Adam Malembeka akikabidhi fedha kwa kikundi cha ujasiriamali cha Amani Group.


 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Angelina Adam Malembeka akikabidhi fedha kwa kikundi cha ujasiriamali cha UWT Jimbo la Tumbatu.

 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Angelina Adam Malembeka akikabidhi fedha kwa kikundi cha ujasiriamali cha Na sisi Tupo.

 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Angelina Adam Malembeka akikabidhi fedha kwa kikundi cha ujasiriamali cha Jitihada.

 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Angelina Adam Malembeka akikabidhi fedha kwa kikundi cha ujasiriamali cha Mkorofi si mwenzetu.

 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Angelina Adam Malembeka akiwa katika picha ya Pamoja na Akina mama waliopokea fedha za vikundi vya ujasiriamali.

 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Angelina Adam Malembeka akitoa nasaha kwa akina mama wa UWT wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika hafla hiyo. 

 MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Angelina Adam Malembeka akisalimiana na akina mama wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.


 AKINA Mama wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwa katika hafla hiyo.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

JUMLA ya Shilingi milioni 3.5 zimetolewa kwa vikundi vitano vya ujasiriamali vya wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Fedha hizo zimetolewa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa huo Mhe.Angelina Adam Malembeka ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake kwa wanawake hao ili waongeze mtaji na kujiajiri wenyewe kwa lengo la kuondokana na changamoto ya umasikini.

Amesema wanawake wanatakiwa kuwa mfano bora wa kumiliki kipato kupitia sekta ya ujasiriamali mbali mbali ikiwemo kilimo, ushoni,ufugaji,ufumaji ususi wa mikeka na vikapu pamoja na biashara ndogo ndogo za kuwaingizia kipato.

Amewataka wajasiriamali hao kuwa wabunifu wa kuzalisha bidhaa zenye soko katika mazingira wanayoishi ili wapate faida kwa mujibu wa mtaji waliouwekeza.

Pamoja na hayo amesisitiza mshikamano kwa akina mama hao na kuzitumia vyema fursa hizo kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi katika vikundi vyao.

Aidha ameweka wazi msimamo wake kuwa ni kutekeleza kwa kasi Ilani ya Chama Cha Mapnduzi ya mwaka 2015/2020 kwa kuhakikisha maeneo yote aliyotoa ahadi katika uchaguzi mkuu uliopita anazitekeleza kwa wakati kabla ya 2020.

Pamoja na hayo amewataka wapuuze na kujitenga na upotoshaji, fitna na kauliza za kutengeneza migogoro ndani ya UWT zinazoenezwa na baadhi ya watu wanaosaka nafasi za uongozi bila kinyume na taratibu za Chama na Jumuiya zake.

Nao wanawake hao waliopokea fedha hizo wamempongeza Mbunge huyo kwa juhudi zake za kuwasaidia akina mama ili waweze kuendeleza vikundi vya ujasiriamali vya kuwasaidia kipato.

Pia wameaidi kuwa fedha hizo watazitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa kwa lengo la kuimarisha vikundi vyao kwa kuongeza mtaji.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni