NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ akiwahutubia
wanafunzi 1,222 waliofaulu kwa kiwango cha daraja la I,II katika mitihani ya
Kitato cha Nne mwaka 2018.
WANAFUNZI wa kidato cha Nne mwaka 2018 waliofaulu daraja la Kwanza na la Pili Zanzibar wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa Zawadi na Chama Cha Mapinduzi Zanzibar |
NAIBU
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ameeleza kwamba
ustawi wa elimu nchini umetokana na matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari
12 mwaka 1964.
Hayo
ameyasema katika hafla ya kuwapatia zawadi Wanafunzi wa kidato cha nne mwaka
2018 waliofaulu kiwango daraja la I,II
kwa shule mbali mbali za Zanzibar, hafla iliyofanyika katika kiwanja cha Afisi
Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja.
Dk.Mabodi
amesema baada ya kufanyika Mapinduzi ya
Zanzibar serikali ya wakati huo
ikatangaza kuwa suala la elimu ni bure sambamba na kuimarisha miundombinu ya
upatikanaji wa elimu kwa wananchi wote bila ubaguzi.
Amesema
Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuenzi Tunu ya Mapinduzi kutokana na mambo mema
yaliyotekelezwa kwa haraka mara baada ya kufanyika mapinduzi hayo na wananchi
wakapata uhuru na kunufaika na fursa ya elimu iliyotolewa kwa ubaguzi kabla ya
mapinduzi.
Ameeleza
kuwa kwa sasa Zanzibar imekuwa ni kitovu cha wasomi na watu wenye taaluma mbali
mbali ambao chanzo cha mafanikio hayo kimetokana na kukua kwa sekta ya elimu
nchini.
Katika
maelezo yake Dk.Mabodi amewapongeza wanafunzi mbali mbali waliofaulu vizuri
masomo yao ya kidatu cha nne pamoja na kuwasihi waliofeli kuwa wasikate tamaa bali
wajiendeleze kupitia sekta ya mafunzo ya amali ili wawe na ujuzi.
Amesema
katika kuunga mkono suala la elimu CCM imeandaa mpango maalum wa kuwasaidia
vijana mbali mbali waliofeli masomo yao katika ngazi tofauti za kielimu ili nao
wapate ujuzi wa kujiajiri wenyewe.
Akizungumza
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed
Mahmoud amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wafaulu vizuri kidato cha
sita na kujiunga na vyuo vikuu.
Amesema
elimu ni jambo muhimu kwa maisha ya binadamu hivyo ni lazima wajitume katika
safari yao ya kutafuta taaluma.
Naye
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bi.Angelina Adam Malembeka
amewasisitiza wanafunzi hao kuwa bado wana safari ndefu ya kutafuta elimu hivyo
waendelee kusoma kwa bidii ili wafikie malengo yao.
Jumla ya wanafunzi 1,222 waliofaulu mitihani
ya kidato cha nne kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili(I,II) wamepatiwa
zawadi mbali mbali na Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza na
kuwahamasisha waendelee kusoma kwa bidii na kufaulu katika ngazi mbali mbali
hadi Vyuo vikuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni