Jumatano, 13 Februari 2019

DK.SHEIN: AZUNGUMZA NA WANA CCM WILAYA YA MFENESINI UNGUJA, TAREHE 13/02/2019



 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi na Wanachama wa CCM Wilaya ya Mfenesini.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akitoa Salamu za Chama Cha Mapinduzi kwa Wanachama na Viongozi wa CCM huko Tawi la CCM Mtoni.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja Ndugu Mohamed Rajab Soud akizungumza katika ziara hiyo huko Tawi la CCM Mtoni.
 BAADHI ya Viongozi na Wanachama wa CCM Mkoa wa Magharibi na CCM Wilaya ya Dimani wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa kasi kubwa.
Amesema dhamira ya Serikali ni kutekeleza kwa ufanisi ahadi zilizoahidiwa katika kampeni za uchaguzi uliopita ili zitekelezwe kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Kauli hizo amezitoa wakati akizungumza na katika ziara yake, mara baada ya kukutana na Viongozi na wanachama wa chama hicho Jimbo la Mfenesini, katika mkutano uliofanyika Tawi la CCM Mtoni.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuzungumza na wanachama na kuangalia utekelezaji wa Ilani pamoja na changamoto zake.
Akizungumza na viongozi hao alisitiza haja ya wana CCM kushikamana na kushirikiana ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kushika Dola katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020.
Amesema CCM inatenda kwa vitendo na sio kutoa ahadi za uongo kwani wananchi wanahitaji huduma bora za kijamii.
Amesisitiza umuhimu wa viongozi kujituma zaidi ili Chama kiwe na  wanachama wengi watakaokipigia kura kishinde kwa kishinde.
Alisema ushindi wa CCM katika uchaguzi huo hauna mashaka, lakini akawataka wana CCM kuongeza juhudi za kuimarisha taasisi hiyo.
Ameweka wazi kuwa anatambua kazi kubwa aliyonayo katika kufanikisha ushindi huo na kuukabidhi kwa Rais ajaye.
Aidha, amewataka Viongozi wa Jimbo hilo kukamilisha ahadi walizoweka kwa wananchi na kuwapongeza wale waliokamilisha ahadi hizo, akiweka bayana kuwa yeye tayari ametekeleza ahadi zote.
Dk. Shein amewakumbusha viongozi na wanachama hao kuwaeleza wananchi yale yote yanayofanywa na Serikali ya CCM, ili kuepuka upotoshaji kutoka kwa viongozi wa upinzani.
Amesema  serikali inaendelea na juhudi zake za kuimarisha sekta za kijamii, ikiwemo afya, elimu, maji na barabara
Kwa upande wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Dk. Abdulla  Juma Mabodi, amempongeza Dk.Shein kwa kuendeleza mfumo shirikishi na Jumuishi baina ya Chama na Serikali.
Amesema CCM Zanzibar inaendeleo kuimarika kutokana na kasi ya viongozi mbali mbali kufanyakazi zao kwa ufanisi mkubwa.
Ameeleza kwa sasa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wanaendelea kuhamasishana kwa lengo la kujijenga kimkakati ili kuweka mazingira rafiki ya ushindi wa mwaka 2020.
Pamoja na hayo Dk.Mabodi ameeleza kwamba kazi kubwa iliyobaki ni ni kila kiongozi ndani ya Chama na Serikali kutekeleza wajibu wake ipasavyo kwa lengo la kuwa karibu zaidi na wananchi ambao ndio wenye ridhaa ya kuweka Serikali madarakani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni