VITI na Meza za kisasa zitakazotumiwa na wanafunzi katika madarasa yaliyozinduliwa katika Shule ya Sekondari Michenzani Pemba. |
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ndugu Mwanamkasi Rajab Aziz(aliyevaa mtandio mweusi) pamoja na wananchi mbali mbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Michenzani Wilaya ya Mkoani Pemba. |
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ndugu Madina Mjaka akitoa maelezo ya kitaalamu juu ya ujenzi wa madarasa hayo katika shule ya Sekondari Michenzani. |
BAADHI ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari na Msingi ya Michenzani Pemba wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa majengo mbali mbali katika shule hiyo, |
NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekitii wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amewakumbusha wazazi,walezi kushirikiana na walimu katika kufuatilia mienendo ya watoto wao pindi wanapokuwa shule na majumbani ili viwango vya ufaulu viongezeke zaidi.
Dk.Shein amesema kwamba wanafunzi wanahitaji uangalizi wa hali ya juu kwa kila madau wa elimu ili kuhakikisha wanapata elimu bora na yenye kiwango kinachostahiki ili wafaulu vizuri katika mitihani yao ya shuleni na ya kitaifa kwa ujumla.
Rai hiyo ameitoa Dk.Shein katika ufunguzi wa jengo la skuli ya sekondari Michenzani, Wilaya ya Mkoani Pemba, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika Wilaya za Pemba mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwa upande wa Unguja.
Dk.Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ameeleza kuwa elimu bora na viwango bora vya ufaulu wa wanafunzi wa ngazi mbali mbali za kielimu vitaongezeka endapo wananchi wataamua kushirikiana ipasavyo na Sekta ya elimu kwa kuwajengea watoto mazingira Rafiki ya kupenda kusoma kwa bidi.
Amesema walimu wana dhima kubwa katika kuwaendeleeza kielimu ya wanafunzi, hivyo akawataka kujikita katika kusomesha kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.
Ameeleza kuwa maendeleo ya nchi yoyote ile hutegemea upatikanaji wa elimu bora kwa wananchi wake, hivyo akasisitiza haja ya walimu kujikita katika ufundishaji na kuepuka kasoro zinarudisha nyuma kiwango cha elimu.
Amewasihi wanafunzi hao kusoma kwa bidi huku wakiepuka kufanya kazi au biashara hali ya kuwa wao bado ni wanafunzi.
Amesema ni kazi ya Serikali kuwajengea mazingira bora wanafunzi kwa kuwapatia huduma zote muhimu, ikiwemo vifaa na madawati.
Ameeleza kuwa Serikali kununua madawati 44,000 kutoka nchini China, na kubainisha kuwa nusu ya samani hizo zimewasili na kugawiwa katika skuli mbali mbali Unguja na Pemba.
Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Mmanga Mjengo Mjawili amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa mazingira bora ya kuwezesha wanafunzi kusoma kwa utulivu bila ya kuwepo na kikwazo chochote hatua inayotakiwa kupongezwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni