Jumamosi, 13 Aprili 2019

MATIKIO KATIKA PICHA ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU UWT Z'BAR WILAYA YA DIMANI LEO TAREHE 13/04/2019.

VIJANA wa Kikundi Maalum cha UVCCM wakimvisha sikafu Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya UWT Wilaya ya Dimani Unguja,kwa ajili ya mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa Kamati ya Utekelezaji na Wanawake wa Wilaya hiyo.

 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akipewa heshima na kukaribishwa katika Ofisi ya UWT Wilaya ya Dimani.

 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akikagua Gwaride la Vijana Maalum wa UVCCM alipowasili katika Ofisi za UWT Kiembesamaki Zanzibar.

 BAADHI ya wanawake wa UWT Wilaya ya Dimani wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo katika mwendelezo wa ziara yake Wilayani humo.

 VIONGOZI mbali mbali wa UWT Wilaya ya Dimani  pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo.

 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo wakicheza wimbo maalum wa wanawake uliopigwa na Kikundi cha Taarab ya 'Wapendanao'  kutoka Mkoa wa Magharib Kichama Unguja.

 MSANII Maarufu wa Wilaya ya Dimani  Kombo Vituko akitoa burudani katika hafla hiyo.


MWENYEKITI wa UWT Wilaya ya Dimani akifungua Kikao.

 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akizungumza na Wanawake wa UWT pamoja na viongozi mbali mbali wa CCM na jumuiya zake.

 Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo  akimkabidhi kadi mwanachama mpya aliyejiunga na CCM kutoka Chama cha ADA-TADEA.

  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo  akimkabidhi kadi mwanachama mpya aliyejiunga na CCM kutoka Chama cha ADA-TADEA.

  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo  akimkabidhi kadi mwanachama mpya aliyejiunga na CCM kutoka Chama cha ADA-TADEA.

 KATIBU wa UWT Mkoa wa Magharib Zuwena akiwatambulisha viongozi mbali mbali katika hafla hiyo.

 KATIBU wa CCM Jimbo la Fuoni Salama Rajab Msinga akitoa maoni yake juu ya uimarishaji wa Jumuiya na Chama Cha Mapinduzi kuelekea mwaka 2020.

 KATIBU wa UWT Jimbo la Mwanakwerekwe  Rehema Kondo Kombo akizungumza katika hafla hiyo.

 MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Amina Khamis Omar 'Mama Afika' akizungumza katika hafla hiyo.

 MWAKILISHI wa CCM  Jimbo la Chukwani akizungumza katika hafla.

MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Dimani Hussein Ali Mjema akitoa salamu za Chama Cha Mapinduzi katika hafla hiyo.

 Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi, Zainab Ali Maulid akizungumza katika hafla hiyo.

  Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Tunu Juma Kondo akikabidhiwa zawadi mbali mbali na wanawake wa  UWT Wilaya ya Dimani Unguja.


 BAADHI ya Wajumbe wa Kamati tekelezaji ya UWT Wilaya ya Dimani wakiwa katika hafla hiyo.

 MAAFISA wa UWT Ofisi Kuu ya Zanzibar wakiwa katika hafla hiyo.








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni