Jumatano, 24 Aprili 2019

CCM MKOA WA MAGHARIB YAENDELEA NA ZIARA YAKE JIMBO LA KIEMBE SAMAKI UNGUJA.

 DIWANI wa Wadi ya Mbweni Unguja Ndugu Maabadi Ali Maulid akitoa maelezo juu ya usambazaji wa mipira ya maji Safi na Salama katika maeneo mbali mbali ya Wadi hiyo.

 KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharib wakikagua Mradi wa Maji Safi na Salama uliotekelezwa chini Mfuko wa Jimbo la Kiembe Samaki katika ziara yao ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.

  Afisa Mipango Manispaa ya Magharib 'B' Ndugu Saumu Daniel Yussuf(hayupo pichani) akitoa ufafanuzi wa miradi iliyotekelezwa na Manispaa hiyo katika Kituo cha Afya cha Kiembe Samaki chini ya Mfumo wa Ugatuzi mbele ya Kamati ya Siasa ya CCM ya Mkoa wa Magharib.


KAMATI ya Siasa ya CCM Mkoa wa Magharib wakikagua Vyarahani vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mahmoud Thabit Kombo kwa Kikundi cha Ujasiriamali cha UWT cha Jimbo hilo huko tawi la CCM Mbweni Matrekta Unguja.


CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Magharibi Unguja kimewataka Viongozi wa Jimbo la Kiembe Samaki kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ili kutatua kwa wakati mwafaka changamoto zinazowakabili Wananchi.

Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Ndugu Mohamed Rajab Soud katika mwendelezo wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Jimbo la Kiembe Samaki.

Amesema pamoja na kutekelezwa kwa miradi mbali mbali ya maendeleo kupitia fedha za mifuko ya maendeleo ya Jimbo hilo bado kupanahitajika juhudi za ziara za kutatua kero za wananchi katika sekta za Afya,Maji Safi na Salama pamoja na miondombinu ya barabara za ndani.

Amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi inayotekelezwa na viongozi hao kama thamani ya fedha zinazotumika zinaendana na miradi inayotekelezwa. 

Amewambia viongozi hao kuwa wahakikishe miradi wanayoitekeleza inasaidie jamii husika badala ya watu wachache.

Aidha amewasihi Wananchi wa Jimbo hilo kuithamini na kuitunza miradi mbali inayotekelezwa kupitia Ilani ya CCM ili iwanufaishe vizazi vya sasa na vijavyo.

"Utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya Jimbo la Kiembe Samaki unafanuyika lakini bado sijaridhika kwa baadhi ya maeneo hivyo wahusika wanatakiwa kuongeza kasi kubwa katika kutatua kero za wananchi.",amesema Mwenyekiti huyo Mohamed.

Naye Diwani wa Wadi ya Mbweni Ndugu Maabadi Ali Maulid amesema katika kutatua kero za wananchi wamejipanga kutekeleza miradi mitatu ikiwemo kujenga minara mitatu mirefu katika visima vya maji safi na salama,kumalizia kuezeka bweni Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiembesamaki pamoja na  matengenezo ya Barabara za ndani kwa kushirikiana na Serikali Kuu.

Naye Afisa Mipango Manispaa ya Magharib 'B' Ndugu Saumu Daniel Yussuf akizungumza katika Kituo cha Afya cha Kiembe Samaki amesema wanaendelea kuimarisha huduma za Afya katika Vituo mbali mbali licha ya kukabiliwa na changamoto za uchakavu wa majengo waliokabidhiwa katika mfumo wa ugatuzi.











Hakuna maoni:

Chapisha Maoni