Jumamosi, 20 Aprili 2019

MATUKIO KATIKA PICHA HAFLA YA JUMUIYA YA MAENDELEO YA VIJANA YA CCM KUTOA VIFAA VYA UJENZI NA SARE ZA WANAFUNZI SKULI YA KIDAGONI KASKAZINI 'A'


 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akipokelewa na Wanafunzi wa Shule ya maandalizi,msingi na Kati ya Kidagoni Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja. 

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akipewa maelezo na Sheha wa Shehia ya Kidoti Makame Suweid Haji  juu ya ujenzi wa Kituo cha Afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi katika kijiji cha Kidagoni.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akikagua Kituo hicho. 

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza na Uongozi wa Kamati ya Maendeleo ya Skuli ya Kidagoni. 

VIJANA mbali mbali wa UVCCM wakishusha mabembea mbali mbali yaliyotelewa na Jumuiya ya Vijana wapenda maendeleo kwa ajili ya wanafunzi wa maandalizi wa Skuli hiyo.


 WAJUMBE mbali mbali wa Jumuiya ya Vijana wapenda maendeleo wakiimba wimbo wa mashujaa  mara baada ya kuwasili skulini hapo.

 WANAFUNZI wa Skuli ya Kidagoni wakisoma utenzi 

 VIJANA wa kundi Maalum la Hamasa kutoka CCM Afisi Kuu wakiwa katika hafla hiyo.

 Mwalimu wa Skuli ya Kidagoni Neema Othman Khamis akisoma risala ya Skuli hiyo.

 VIJANA wa kikundi cha sarakasi cha UVCCM Wilaya ya Kaskazini 'A' wakionyesha uwezo wao katika hafla hiyo.


VIJANA wa kundi Maalum la Hamasa kutoka CCM Afisi Kuu wakiwa katika hafla hiyo.
 MJUMBE wa Jumuiya ya Vijana wapenda Maendeleo akisoma risala ya Jumuiya hiyo.

 MWENYEKITI wa  Jumuiya ya Vijana wapenda Maendeleo Mwinyi Ahmed Mwinyi akizungumzia lengo la kutoa vifaa vya ujenzi pamoja na sale,viatu,mikoba na mabembea kwa wanafunzi wa Jumuiya hiyo.

 MWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Kaskazini 'A' akitoa salamu za CCM katika Wilaya hiyo.

 KATIBU wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mulla Othman Zubeir akitoa salamu za CCM kwa niaba ya Mkoa.

 MWAKILISHI  wa Jimbo  la Nungwi Mhe. Ame Haji Ali akizungumzia utekelezaji wa Ilani katika Jimbo hilo mbele ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.

  MWENYEKITI wa  Jumuiya ya Vijana wapenda Maendeleo Mwinyi Ahmed Mwinyi akikabidhi Sale za wanafunzi ambavyo ni moja vitu mbali mbali vilivyotolewa na Jumuiya yake kwa Skuli ya Kidagoni.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwahutubia wananchi wa Kidagoni katika hafla hiyo.



 PICHA ya pamoja ya viongozi wa Jumuiya, Viongozi wa Skuli ya Kidagoni pamoja na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa na Ujumbe wa Viongozi mbali mbali wa CCM na Jumuiya zake kutoka Kibiti na Rufiji.(PICHA NA IS-HAKA OMAR-AFISI KUU YA CCM ZNZ).






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni