katibu wa
UWT wilaya ya Mjini akizungumza na baadhi ya viongozi na wa jumuiya hiyo wakati
wa makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya kituo cha elimu amali UWT
wilaya ya mjini uliotolewa na mbunge wa viti maalum ccm mkoa wa mjini Asha
Abdulla Juma.
MBUNGE wa viti maalum wa Mkoa wa Mjini,Mhe Asha Abdulla Juma amefurahishwa na hatua ya Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi ya wilaya ya Mjini kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi kwa kuhakikisha vijana wanajikwamua kiuchumi.
Amesema kitendo cha UWT kuwakusanya vijana tofauti ndani ya mkoa huo kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali ili waweze kuondokana na hali ya utegemezi ambapo baadaye wakipata ujuzi wanajishughulisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kujiingizia kipato ni moja ya sehemu ya maagizo ya ilani pamoja na viongozi wa chama.
Kauli hiyo ameitoa wakati akikabidhi vifaa vya ushonaji ikiwemo chereheani mbili,meza pamoja na vitambaa vya kutengeneza mapambo katika kituo cha mafunzo ya amali cha UWT wilaya ya mjini ambapo alisema hiyo ni ahadi za CCM katika kuwakusanya vijana na kuwajengea uwezo wa kujitegemea na kuondokana na utegemezi.
Amesema baada ya kuona Jumuiya hiyo imeanzisha kituo hicho cha mafunzo kwa ajili ya vijana akaiona aunge mkono juhudi hizo za kuhakikisha vijana hao wanaokombolewa dhidi ya ukosefu wa ajira ili kuongeza uzalishaji nchini kama maagizo ya viongozi wa CCM wanavyoelekeza.
"Nina amini chuo hichi kitasaidia sana juhudi hizi kwa vijana wetu na ndio maana nikaona nilete nguvu kwenye kituo hichi cha UWT hasa kwa wakina mama katika kujifunza ujasiriamali wa ushonaji,upishi na mambo mengine,"ameeleza
Naye Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mjini,Habiba Nassir Suleiman amesema lengo la uongozi wa wilaya hiyo ni kuendelea kubuni miradi itakayosaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa ajira na ongezeko la uzalishaji kwa lengo la kukuza uchumi kama inavyoelekeza CCM.
Amesema uongozi wa UWT wilaya imeamua kufanya ubunifu wa aina hiyo wa kuwakusanya vijana na kuwapatia mafunzo ya ujuzi wa shughuli za ujasiriamali ambapo kwa namna moja ama nyingine itawasaidia sana wanawake katika kuondokana na hali ya utegemezi na kuweza kujikwamua kiuchumi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni