MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita akizungumza katika hafla ya mapokezi hayo kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti. |
MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)Taifa,
Tabia Maulid Mwita amewataka vijana
kuvunja makundi yote yaliyoundwa wakati wa kampeni za uchaguzi na badala yake
libaki kundi moja la UVCCM litakalotetea na kusimamia maslahi ya vijana wote wa
Tanzania.
Rai hiyo ameitoa leo katika hafla ya mapokezi ya viongozi wa
jumuiya hiyo ngazi ya Taifa waliofika Zanzibar kwa mara ya kwanza tokaka
wachaguliwe kupitia Mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM uliofanyika wiki kadhaa
zilizopita Mjini Dodoma.
Amesema uchaguzi umekwisha na tayari viongozi wa ngazi mbali
mbali wamechaguliwa hivyo kilichobaki kwa viongozi hao ni kuwatumikia vijana wa
Umoja kwa ufanisi.
Amesema changamoto zinazoikabili UVCCM zitatafutiwa ufumbuzi
wa kudumu endapo vijana mbali mbali wa umoja huo watakuwa tayari kushirikiana
na viongozi wao katika kutathimini na kubuni mikakati mipya ya kuleta
maendfeleo ndani ya umoja huo.
“ Ndugu zangu wapendwa na vijana wenzangu wa UVCCM
nakupendeni sana lakini ushauri wangu kwenu ni kwamba tufanye kazi kwa bidii
ili umoja wetu uendelee kuwa na heshima ya ndani na nje ya Chama cha Mapinduzi.
Pia uchaguzi umekwisha lakini pia makundi ya kuharisha uhai
wa jumuiya yetu, rushwa na ufisadi tuyapige vita kwani hayatatusaidia bali
yatatutafuna na kudhohofisha taasisi yetu.”, amesema Makamu Mwenyekiti huo.
Hata hivyo amewashukru vijana mbali mbali wa umoja huo
wanaoendelea kuonyesha upendo na mshikamano kwa uongozi mpya wa ngazi ya taifa
uliochaguliwa kuongoza kwa miaka mitano ijayo.
Amewambia mamia ya vijana waliojitokeza katika mapokezi hayo
kwamba Umoja huo umejipanga kufanya mageuzi makubwa katika masuala ya uongozi na kiuchumi kwa lengo la kufanya
taasisi hiyo kuwa kimbilio la kudumu kwa vijana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni