Jumapili, 24 Desemba 2017

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI ZA MATUKIO YA MAPOKEZI YA DK. SHEIN


MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la  Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia katika hafla ya mapokezi yake yaliyofanyika leo katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja.

 BAADHI ya Wanaschama wa CCM walioudhuria katika Hafla hiyo

 MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Balozi Seif Ali Iddi( kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib(kulia) hafla ya mapokezi ya Dk. Shein.

 VIONGOZI mbali mbali wa Chama na serikali walioudhuria hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla Mabodi(kulia mwanzo), Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambayepia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kulia wa pili), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Mkuu wa Mkoa wa Mjini na Magharib Ndg. Ayoub Mahmoud 

 KIKUNDI cha Brass Band cha UVCCM kikiendelea kutekeleza majukumu yake katika hafla hiyo.

 VIJANA wa Chipukizi wakimvisha sikafu Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika mapokezi yake.

 Baadhi ya viongozi wa CCM wakiongozwa na Dk. Shein wakiwa katika hali ya ukakamavu baada ya kuibwa wimbo maalum wa chama cha mapinduzi kwa ajili ya shughuli hiyo.

 Dk.. Shein akiwa na Mama Mwana Mwema Shein wakisikiliza burudani ya ngoma maarufu ya kibati mara baada ya kuwasili katika viwanja vya CCM Mkoa mjini Unguja.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla Mabodi(kushoto) akibadilishana mawazo na  Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar
Dk. Ali Mohamed Shein katika hafla hiyo

 KIKUNDI cha ngoma za asili cha imarisha wakitoa burudani kwa
Mgeni Rasmi na waalikwa wa hafla hiyo.


 KIKUNDO Cha Taarab cha Big Star kikitoa burudani mara tu baada ya
Dk. Shein kuingia ukumbini kwa ajili ya mapokezi yake.

 BAADHI ya  viongozi wastaafu wa Chama na Serikali akiwemo Waziri kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Mhe. Shamsi Vuai Nahodha pamoja na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar, Mzee Ali Ameir Mohamed wakiwa katika hafla hiyo.

 BAADHI ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakipiga makofi na kuimba nyimbo mbali mbali za Chama  ikiwa ni ishara ya mapokezi ya Dk. Shein.

 VIONGOZI mbali mbali wa Chama wakiongozwa na Dk. Shein  wakiimba katika hafla hiyo.


 Msoma Qur-an Tukufu Ndg Yussuf Abdullah Nassor |( Bayuu ) 
akisoma Aya mbali mbali zinazoendana na hafla hiyo

 MSOMA utenzi Farida Rajab  akisoma utenzi katika hafla hiyo,

 BAADHI ya wanachama na Viongozi wa chama cha Mapinduzi walioudhuria katika hafla hiyo.

 Katibu msaidizi Mkuu  Idara ya Itikadi na  Uenezi CCM Zanzibar,
Daud Ismail Juma akisoma risala ya Wana CCM wa Mikoa Sita  kichama  Zanzibar. 

 Mwenyekiti wa Mkoa Kusini Unguja, Ramadhani Abdallah Ali
akitoa salamu za Wenyeviti wa Mikoa Sita Kichama katika hafla hiyo.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saadalla Mabodi
akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo.



 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mjini, Talib Ali Talib akizungumza
 kwa niaba ya  Wana CCM wa Mkoa huo.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni