Alhamisi, 21 Desemba 2017

CCM YAUNDA TUME KUTATHMINI MALI ZAKE NCHI NZIMA.

 VIONGOZI Wakuu wa Chama cha Mapinduzi.


CHAMWINO, DODOMA.

Chama  Cha Mapinduzi (CCM) kimeunda Tume itakayofuatilia mali zake zote zilizopo nchini kote. 

Tume hiyo imeundwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kilichofanyika jana Ikulu ya Chamwino nje kidogo ya mjini Dodoma. 

Timu ya Tume hiyo iliyoteuliwa katika kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM  Rais Dk. John Magufuli Mwenyekiti wake ni

Dk. Bashiru Ali Kakurwa na Wajumbe ni, 

1. Walter Msigwa

2. Albert Msando

3. Galala Wabanhu Hananasifu

4. Albert Chalamila

5. William Sarakikya

6. Komanya Kitwara

7. Dk. Fenela Mkangara

8. Mariam Mungula

Moja ya majukumu iliyopewa tume hiyo ni kuzunguka nchi nzima kuziona zilipo mali zote za Chama na kuzifanyia uratibu na tathmini. 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni