KAIMU Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, amesema
licha ya Umoja huo kupita katika misukosuko na mawimbi makubwa ya changamoto za
kisiasa na kiutawala lakini bado viongozi wake wamebaki imara na wenye misimamo
isiyopinda katika kusimamia maslai ya vijana.
Hayo ameyabainisha leo wakati akizungumza katika hafla ya
mapokezi ya viongozi wa UVCCM Taifa waliofika Zanzibar leo kwa mara ya kwanza
toka wachaguliwe kupitia Mkutano Mkuu wa Umoja huo uliofanyika hivi karibuni.
Shaka amesema Umoja huo umepitia katika kipindi kigumu cha
misukosuko ambayo wakati mwingine iliwayumbisha baadhi ya viongozi lakini
baadae wakarudi katika mstari ulionyooka kutokana na nasaha za viongozi wa CCM.
Ameeleza kuwa maendeleo endelevu ya umoja huo yataletwa na
vijana wenye nia, maono na uzalendo wa kweli katika kujenga hoja zenye uhalisia
wa kuisaidia jumuiya hiyo na sio kuibomoa.
“ Namshukru mungu toka nimekuwa kiongozi ndani ya umoja huu
nilipoanzia Zanzibar hadi kuteuliwa na kuhamishiwa Tanzania bara kwa wanaoijua
UVCCM nilivyoikuta wanakiri kuwa kwa sasa ina maendeleo kuliko ilivyokuewa
wakati wa nyuma.”, amefafanua Shaka.
Shaka amesema huu sio wakati wa maneno na porojo bali ni muda
mwafaka wa kila kijana kutumia elimu, maarifa na mbunu mbadala katika kuishauri
jumuiya iweze kufanya mambo mazuri yenye tija kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa
ujumla.
Ameahidi kuwa ataendelea kushirikiana na vijana wote bila
kujali tofauti za kijinsia, umri, rangi,kabila na dini kwa lengo la kuhakikisha
malengo ya UVCCM yanatimia kwa asilimia 100 kabla ya mwaka 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni