Alhamisi, 14 Desemba 2017

MATUKIO KATIKA PICHA MAPOKEZI YA VIONGOZI WAPYA UVCCM TAIFA NA MAPOKEZI YA VIONGOZI NA WANACHAMA 200 KUTOKA UPINZANI NA KUJIUNGA NA CCM

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndg:Kheir Denice  James (katikati) akiwasili Ofisi za Makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (kushoto)Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka.
 VIONGOZI mbali mbali wa Chama na Mapinduzi na UVCCM wakifuatilia matukio mbali mbali yanayoendelea katika mapokezi ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa katika Mkoa wa Dodoma yaliyoambatana na kupokea wanachama wapya 200 kutoka vyama vya upinzani.
 BAADHI ya wanachama wa CCM walioudhuria katika hafla ya Mapokezi ya Mwenyekiti wa UVCCM  Taifa, Kheri James yaliyofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM-Dodoma.



 MWENYEKITI wa UVCCM Mkoa wa Dodoma Bill Chidabwa akiwakaribisha wageni na viongozi  mbali mbali wa Mkoa huo katika hafla hiyo.

 KAIMU Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akimkaribisha  Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Tabia Maulid Mwita ili awasalimie Wana Dodoma.

 MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Tabia Maulid Mwita akizungumza na mamia ya Wana CCM na wananchi walioudhuria katika mapokezi ya viongozi wapya wa ngazi ya Taifa wa Umoja huo waliochaguliwa hivi karibuni.

 MWENYEKITI wa UVCCM Taifa, Kheir Denice James akihutubia katika hafla ya mapokezi ya viongozi hao yaliyoandaliwa na UVCCM  Mkoa wa Dodoma.

 ALIYEKUWA  Afisa wa sheria wa ACT Wazalendo Mwantumu Mgonja na amejiunga na CCM (kushoto) akipongezwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheir Denice James  katika hafla hiyo iliyoambatana na mapokezi ya wanachama wapya 200 kutoka upinzani wakiwemo viongozi wa ngazi za juu.
 ALIYEKUWA Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Mwanza  Robert Gwanchele na amejiunga na CCM  (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheir  Denice James.
ALIYEKUWA  msanii wa CHADEMA  na amejiunga na CCM,  Andrew Mgalama(kushoto) akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Tabia Maulid Mwita.
Katibu Mipango na Uchaguzi ACT Wazalendo  Wilaya ya Tarime Pascal Warioba na amejiunga na CCM, akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Kheir  James Denis.

 ALIYEKUWA Mwenyekiti wa chama hicho Jimbo la Singida Mjini, Nkamia John na amejiunga na CCM(kushoto) akisalimiana na Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole pamoja na Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni Makao Makuu ya CCM, Pereira Ame Silima.
 BAADHI ya  viongozi na wanachama waliohama vyama vya upinzani vikiwemo CUF, CHADEMA na ACT-Wazale na kujiunga na CCM wakiwa mbele ya meza kuu kwa ajili ya kupokelewa rasmi.
 Anthon Mrigini Katibu wa Vijana Wilaya ya Tarime, Yaassin Daud(katikati)  Julius Sinda Katibu wa CUF Wilaya ya Tarime(kushoto) waliojiunga na CCM wakibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk. Abdalla Juma Mabodi mara baada ya mapokezi ya wanachama hao.
 MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM Taifa, Haidar Haji Abdalla (kushoto) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi katika hafla ya mapokezi ya viongozi wapya wa UVCCM taifa iliyofanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM Taifa Dodoma.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni