Jumamosi, 23 Desemba 2017

DK.SHEIN AWAPA ZAWADI YA KIHISTORIA TIMU YA ZANZIBAR

Timu ya Zanzibar Heroes.


RAIS  wa Zanzibar ametangaza zawadi mbili alizowahidi wachezaji na viongozi wa Zanzibar Heroes hivi punde katika sherehe aliyowaandalia.

Zawadi hizo ni kama ifuatavyo:


•Kila mchezaji atapewa shilingi milioni tatu taslimu, fedha ambazo kila mmoja ataangiziwa          kwenye account yake ya benki.


• Kila mchezaji atapewa kiwanja kwa sharti la kutouza viwanja hivyo na vitakua pamoja

Wakati huo huo Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein amekubali maombi ya kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes Hemed Suleiman Moroko ya kutaka amualike Rais wa chama cha soka cha Afrika Ahmad Ahmad kuja Zanzibar kujionea hali ya mpira wa Zanzibar.

Rais Shein ameyakubali maombi hayo na amesema atamualika Rais huyo kuja Zanzibar kujionea soka la Zanzibar na pia kuweza kumshawishi kuweza kuirejeshea Zanzibar uwanachama wa CAF.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni