Jumatatu, 18 Desemba 2017

ROSE MHANDO AOMBA UANACHAMA WA CCM.

 MWANAMZIKI wa nyimbo za injili Tanzania Rose Mhando.

BAADA  ya kuwa kimya kwa muda mrefu, mwanamziki wa nyimbo za injili nchini Rose Mhando ametumbuiza katika mkutano wa tisa wa CCM Taifa  uliofanyika mjini Dodoma, kisha kuomba kujiunga na chama hicho tawala.

Awali Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Humphrey Polepole akimkaribisha jukwaani kutumbuiza, aliwatangazia wajumbe wa mkutano kuwa Rose Mhando na kundi lake atapanda jukwaani kutumbuiza na baada ya hapo, atawasilisha ombi lake la kutaka kujiunga na chama hicho tawala.

Rose aliimba wimbo wa kusifu utendaji wa Rais John Magufuli na kibwagizo kinachomalizikia na maneno .”tuna imani nawe.” Rose Mhando, alipomaliza shoo’ yake,wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa yote hapa nchini waliinua mabango yao na kumshangilia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni