Jumanne, 12 Desemba 2017

MATUKIO KATIKA PICHA MKUTANO MKUU WA TISA WA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA-2017



 BAADHI ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu huo wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni rasmi Dk.John Pombe Magufuli.

 KAIMU Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (kushoto) Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Tabia Maulid Mwita(kulia) wakiwa Katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja wa Wazazi CCM uliofanyika leo ukumbi wa JK Convetion Centre-Dodoma.
 Kikundi cha burudani cha TOT kikiongozwa na malkia wa mipasho Khadija Kopa wakitoa burudani wakiwa na wajumbe waliobeba mabango ya Mikoa yao katika Mkutano huo

 BAADHI ya Wajumbe wa Vyama vya upinzania ambavyo ni marafiki wa CCM(waliokaa mstari wa mbele) wakifuatilia matukio mbali mbali yanayoendelea katika ukumbi wa Convetion Centre- Dodoma katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa CCM Tanzania.
 BAADHI ya Wazee wa Chama cha Mapinduzi waliowahi kuhudumu katika Umoja huo na kushika nyadhifa mbali mbali katika Chama na Serikali wakiwa katika Mkutano huo.
 MKE wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Mama Fatma Karume akiwa ni mmoja wa wazee walioalikwa katika Mkutano huo.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni