BAADHI ya Wazee wa Chama cha Mapinduzi walioudhuria Mkutano Mkuu. |
MKUU wa Mkoa wa Njombe Chrispher Ole Sendeka(kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Mzee January Makamba (kulia). |
MANAIBU Makatibu wakuu wastaafu wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia matukio mbali mbali yanayoendelea katika Mkutano huo. |
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu huo kutoka Zanzibar wakiwa katika Mkutano Mkuu huo. |
VIONGOZI wa Vyama vya upinzani walioalikwa katika Mkutano Mkuu huo kwa lengo la kuongeza mahusiano ya kisiasa. |
BAADHI ya wake wa viongozi walioshiriki katika mkutano huo. |
BAADHI ya Maspika wastaafu wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Baraza la wawakilishi Zanzibar wakibadilishana mawazo katika Mkutano Mkuu wa tisa wa CCM Taifa. |
WAJUMBE wa Baraza la Wadhamini la Chama cha Mapinduzi walioshiriki katika Mkutano Mkuu huo. |
BAADHI ya wanachama na viongozi wa zamani wa vyama vya upinzani waliojiunga na CCM hivi karibuni. |
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi za elimu ya juu na makundi maalum walioudhuria mkutano huo |
KATIBU Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Omar Kinana akitoa taarifa ya utekelezaji ya chama cha mapinduzi ya miaka mitano iliyopita. |
BAADHI ya wasanii wa Bongo movie ambao ni wanachama wa CCM walioshiriki katika Mkutano Mkuu huo. |
MAKAMU Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Tabia Maulid Mwita akiwa ni miongoni mwa wajumbe walioshiriki Mkutano Mkuu huo. |
KUNDI la wagombea wa NEC, viti 15 kutoka Zanzibar. |
MWENYEKITI wa Baraza la vyama vya siasa Tanzania, John Shibuda akitoa salamu za vyama hivyo katika mkutano Mkuu huo. |
Mwanasiasa Mkongwe wa Chama cha UDP, Mzee John Cheyo akizungumza katika mkutano mkuu huo. |
BAADHI ya Wajumbe na Wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi kwa ngazi ya taifa wakifuatilia mkutano Mkuu huo. |
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya utekelezaji ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. |
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiduzi, Balozi Seif Ali Idd akisoma taarifa ya utekelezaji kwa upande wa Zanzibar. |
BAADHI ya wagombea wa kundi la NEC, viti 15 kutoka Zanzibar. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni