MWASISI wa Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964, Brigedia Jenerali Mstaafu Ramadhani Haji Fakii(kushoto) akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Mwita(kulia) alipofika nyumbani kwake Maisara Unguja kwa ajili ya kumtembelea.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMU wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha
Mapinduzi (UVCCM), Tabia Mwita amemtembelea Brigedia Jenerali mstaafu Ramadhani Haji Faki,
ambaye ni miongoni wa wanamapinduzi 14 waliofanikisha Mapinduzi ya mwaka 1964.
Brigedia Jenerali Faki
kati ya wanapinduzi hao 14 ndiye aliyebakia hai na pia alikuwa Waziri Kiongozi
wa kwanza katika Baraza la Mapinduzi baada
ya Mapinduzi hayo kutokea.
Akizungumza nyumbani
kwake baada ya kutembelewa na Makamu huyo Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia, Mwanapinduzi
huyo amesema kuna umuhumi wa kuhakikisha vijana wa sasa kuyaenzi na kulinda
dhana ya mapinduzi hayo yaliyotekelezwa na vijana wa enzi za ASP.
"Nilimwambia Mzee Abeid Amani Karume kuwa lazima tuipindue
serikali ya Sultan kwani ilikuwa wakiwadhalilisha Waafrika ambao ni wazawa na namshukru mungu mipango yetu
ikafanikiwa toka mwaka 1964 Zanzibar
ilikuwa huru kiuchumi, kijamii, kimaendeleo na kisiasa.,"alisema.
Mwanapinduzi huyo amesema baada ya kuipindua serikali ya Kisultani serikali
ya Mapinduzi ilitangaza kuwa elimu ni bure na wananchi walihimizwa kusoma
kutokana uamuzi wa serikali ya mapinduzi kutangaza bure ili kupata wataalamu wa
kuiletea nchi maendeleo.
Faki alimtaka Makamu Mwenyekiti huyo ambaye ni kamanda mkubwa
wa vijana Tanzania kuhakikisha vijana nchini wanapaswa kuyalinda kwa hali na
mali.
"Sidhani kuwa kama kuna mtu atakuja kuyapindua Mapinduzi
haya na kwamba labda ayafanyie nchi nyingine na si Zanzibar mapinduzi haya ni
ya mwisho na sifikiri tena kama kuna mtu atakuja kuyafanya mapinduzi
mengine,"alisema Faki.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti huyo Tabia, amemuhakikishia
Mwanapinduzi huyo kuwa UVCCM itahakikisha yanayalinda mapinduzi hayo ambayo yalitokea mwaka 1964.
Amesema amejifunza
mambo mengi kutoka kwa mwanamapinduzi huyo ambapo amebaini umuhimu wa kuwatumia
vijana kuwafunza kuwa katika hali ya uimara na uzalendo mkubwa kwa kuyalinda
mapinduzi hayo.
"Nikiwa mimi ni Makamu Mwenyekiti wa UVCCM,ninawaeleza
vijana wenzangu kuwa hakutatokea Mapinduzi yeyote isipokuwa kuyaendeleza na
kuyawekea mipango ya kufanya kuleta
maendeleo,"alisema
Makamu huyo amesema kupitia UVCCM mpya ambayo ni imara
itaendelea kuyadumisha na kwamba yasifanyike mambo yakaleta fikra ya kutokea
kwa mapinduzi mengine wakati yalishafanyika kwa mwaka 1964.
"Leo nimeona na nimesisimuka sana baada ya kupata
historia ya kutokea kwa mapinduzi haya na kwamba yalikuwa lazima kutokea
kutokana na unyama wa serikali ya Sultani aliyafanya na udhaifu wa kuongoza
serikali,"alisema.
Tabia amefafanua kuwa
amekuja kujifunza taarifa za ndani za mahusiano ya ndani kati ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM), kilipotoka na kinapoelekea na kutoka Chama cha Afro shiraz Party
(ASP) na TANU hadi CCM na kwamba elimu aliyopata ni umuhimu wa uzalendo kwa vijana katika kutetea
nchi kwa kujitolea.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni