NA IS-HAKA
OMAR, DODOMA.
NAIBU Spika wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson Mwansasu amesema UWT itavuka
vikwazo vya kisiasa na kiuchumi endapo viongozi na watendaji wa umoja huo wa
ngazi za juu watakuwa tayari kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi wa
ngazi za chini.
Rai hiyo
ameitoa leo wakati akizungumza katika mapokezi ya viongozi wa UWT ngazi ya
Taifa yaliyofanyika leo katika viwanja vya White house Makao Makuu ya CCM
Dodoma.
Amesema umoja
na mshikamano ndio nyenzo ya kuimarisha Umoja huo wenye jukumu la kuwaunganisha
wanawake na kusimamia malezi ya vijana hasa wa kike.
Amewasihi
wanawake nchini kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono mafanikio yanayoletwa
na usimamizi mzuri wa Sera imara za CCM.
" Wanawake
ni hazna ya CCM kisiasa na kiuchumi hivyo tuonyeshe uwezo wetu kama tunaweza
kweli kuleta maendeleo endelevu wenyewe bila ya kusimamiwa na mtu yeyote bali
tujiongoze na kujisimamia wenyewe", amesema Dkt.Tulia.
Mwanataaluma
huyo wa Sheria ameeleza kwa kuongeza kwamba anaona ishara ya mafanikio kupitia
viongozi wa UWT waliochaguliwa kwa ngazi zote hasa taifa kwani wote ni
wachapakazi na wenye wivu wa maendeleo.
Amewakumbusha Akina mama hao kuwa mara baada
kupatikana viongozi hao kazi iliyobaki ni kuijenga UWT ili iwe kituo cha
matumaini ya Wanawake wa Tanzania nzima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni