Jumatatu, 4 Desemba 2017

CCM YATEKELEZA AHADI HUKO UKUNJWI, PEMBA

Na Is-haka Omar, Zanzibar.
         
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewahakikishia wanachama wake na wananchi kwa ujumla kuwa kitaendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi mbali mbali zinazotolewa na Chama hicho katika jamii.  
                                          Akizungumza  Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar , Waride Bakari Jabu wakati akikabidhi fedha kwa wanachama wa CCM ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu Dk. Abdulla Juma Mabodi ,  mwezi Julai mwaka huu katika Shehia ya Ukunjwi Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Amesema CCM ina utamaduni wa kutekeleza ahadi kwa  zake kwa wakati ili wananchi wapate huduma bora za kijamii,kisiasa na kiuchumi.

Amewaeleza wanachi wa kijiji hicho kwamba wakati wa kufanya siasa za maneno matupu umekwisha na kwa sasa wananchi wanahitaji  huduma muhimu zitakazowaletea maendeleo.

“ Ungwana ni vitendo  na Chama cha Mapinduzi  kinatenda kwa vitendo kuliko maneno na huo ndio msingi wa falsafa ya Sera zetu toka enzi za waasisi wa ASP na TANU.

Furaha ya Chama chetu ni kuona wananchi wananufaika na huduma muhimu za kijamii zinazotolewa na serikali kwa lengo la kuwaondosha katika wimbi la umasikini.”, amesema Waride.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa serikali ya awamu ya saba chini ya uongozi wa Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, imeimarisha huduma mbali mbali za Afya, Elimu na miundombinu ya barabara kwa lengo la kuwasogezea karibu huduma za kijamii wananchi wa kisiwa hicho.

Amewataka wanachama wa CCM Kisiwani humo kuishi kwa amani na kujiamini  huku wakijivunia kuwa miongoni mwa mamia ya wanachama wanaoamini na kuunga mkono Sera, itikadi na miongozo mbali mbali ya Chama cha Mapinduzi.

Hata hivyo, amewasihi wafuasi na wanachama waliopo ndani ya Chama cha CUF  kujiunga na CCM ili waweze kunufaika na mfumo wa siasa huru zinazojali haki na misingi ya kidemokrasia kwa kila mtu.

Aidha amewasisitiza  viongozi wa Chama ndani ya Mkoa huo kuhakikisha fedha zilizotolewa zinatumiwa kwa mahitaji yaliyokusudiwa ili kupata Tawi la kisasa linaloendana na hadhi ya CCM.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu yupo kisiwani Pemba kwa ajili ya shughuli maalum za utekelezaji wa majukumu ya Chama cha Mapinduzi.

Katika hafla hiyo Katibu huyo amekabidhi fedha taslim shilingi milioni milioni 1,700,000 kwa ajili ya ujenzi wa Tawi la CCM lililopo katika Shehia ya Ukunjwi.


Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar  Waride Bakari Jabu, akibadilishana mawazo na viongozi wa CCM  Mkoa wa Kaskazi Pemba katika hafla ya kukabidhi fedha za Tawi la CCM huko Ukunjwi.

 Baadhi ya Wanachama wa CCM katika Kijiji cha Ukunjwi Pemba wakiwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar  Waride Bakari Jabu wakielekea katika jengo la Tawi la CCM.



 Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,  Zanzibar  Waride Bakari Jabu akiwa na fedha kwa ajili ya kuzikabidhi kwa viongozi wa Tawi la CCM lililopo Ukunjwi, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni