MWENYEKITI wa UVCCM Taifa Kheir Denice James akihutubia katika hafla ya mapokezi ya viongozi wapya wa Umoja huo ngazi ya Taifa yaliyoandaliwa na UVCCM Mkoa wa Dodoma. |
NA IS-HAKA OMAR, DODOMA.
MWENYEKITI mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM )
Kheir Denice James amesema atahakikisha anasimamia kwa nguvu zake zote
madhumuni, kanuni, dira na malengo ya jumujiya kipindi cha mwaka 2017 hadi 2022
kwa nia ya kuleta ustawi na mageuzi mukubwa ndani ya UVCCM.
Amesema anajua kuwa ada na ujira wa kusema kweli huwa
haupendwi na wengi ila yeye huona raha na fahari kusema kweli hata kama ukweli
huwa unauma.
Mtamshi hayo ameyatoa jana kwenye hafla fupi
alipozungumza na wana UVCCM kwenye viunga vya Makao Makuu ya CCM White
House mkoani hapa.
Kheir
alisema mpango na mkakati wa serikali katika utoaji wa asilimia 5 kwa vijana na
wanawake si hisani wala fadhgila hivyo halmashauri ambazo bado zinasuasiuua
katika utoaji wa fedha hizo zihakikishe zinatimiza wajibu huo.
Alisema
ikiwa mkurugenzi wa halmashauri yoyote nchini anaona uzito wa kutoa asilimia
hizo kwa vijana na wanawake ni viziri akamueleza Raia kama kazi aliyopewa
imemshinda ili aqweze kukaa pembeni.
"Asilimia
hizo lazima zitoke ili kuwasaidia vijana kujiendelkeza kimiradi na kujipatia
vipato vyuao kiuchumi.Ikiwa tutaamua kunyamaza iko siuku tutyapigwa mawe kwa
kushindwa kuwasaidia vijana wakati serikali imeweka utaratibu mzuri wa utoaji
wa mikopo hiyo" Alisema Kheir.
Aidha
aliwapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM kwa uwamuzi wao wa kumchagua na
kuwa Mwenyekiti wa jumujiya ya Vijana ya chama cha mapinduzi huku akipiga
marufuku kwa mwanachama asiye na dhamana ya kimamlaka kuisemea jumuiya.
Mwenyekiti
huyo mpya wa UVCCM alisesma kuanzia sasa kiongozi atakayekuwa akiisemea jumuiya
ni yule mwenye mamlaka ya kikanuni na kikatioba akiwemo Mwenyekiti wa jumuiya ,
katibu mkuu,Makamu mwenyeiti ,wenyeviti wa mikoa na wilaya sio vinginevyo.
Pia
aliwataka vijana ambao bado wako upinzani kurudi haraka ndani ya chama tawala
kwani kubaki kwao nje hakjuitaweza kuwasaidia kutokana na vyama vyao kuwa
vichanga na havina uwezo wa kuiondoaha ccm madarakani.
"Asiyeungana
na CCM sasa ni kama mtu anayepishana na gari lenye mishahara.Yeye wakati
anatokna nje gari la mishahara linaingia ndani,Tutaendelea kuwaeleimisha vijana
wenzetu kewas kusimamia malengo yretu,kuonyesha umoja,mshikamano bila ya
kugonganagongana"Alieleza Kheir.
akizungumzia
rasilimali na mali za chama ,Mwenyekiti huyo wa UVCCM alisema kabla makao makuu
haijaikagua mikoa ,wilaya na kata watendaji katika ngazi hizo ni vyema
wakajikagua wao wenyewe na kuaninisha ipo miradi mingapi,majengo na vitega
uchumo.
"Nataka
kujua mali,vitega uchumi na rasilimali za jumuiya kuanzia zanzibar
hadi Tanzania Bara na kila kitu kionyeshwe kinavyozalisha tija na faida
zake kwa njia za uwazi bila kujkjitokeza ubabaishaji"Alisisitiza.
Hata
hivvyo alisema wakati wa aina ya wanachama vibaraka na wasaliti kubaki
ndani ya chama au kwenye jumnuiya za chama umekwisha hivyo ni lazima wajulikane
na kutoswa mara moja.kweani wakiachwa ni hatari kwqa chama na utawi wake.
Akielezea
suala la kuimarisha nidhamu na maadili,Kheir alisema wale wote ambao
wanakishambulia chama kwenye mitandao ya kijamii kwasababu za kipuuzi ili
kukidhoofisha wa watanyooshwa kwa kutiwa adabu.
"Hiwezekani
mtu awe analipwa mshahara na serikali za ccm au jumuiya zake kisha yeye awe
kiranja wa kukivuruga chama au jumuiya kwa kuandika uopngozo na uzushi kwenye
mitandao na mtu huyo aachwe akitamba"Alionya.
Kwenye
hafla hiyo jumla ya wanachama 200 toka vyama vya upinzani wengi wakiwa ni
kutoka ACT Wazalendo,Chadema na CUF wamejiunga na CCM na kupewa kadi mpya za
uanachgama akiwemo aliyekuwa Afisa wa kitengo cha sheria ACT Wazalendo
Mwamtumu Mgonja na Mkurugenzi wa siasa wa chama hicho Mkoa Mara Pascal
Warioba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni