Jumatatu, 11 Desemba 2017

MATUKIO KATIKA PICHA YA MKUTANO MKUU WA TISA WA UVCCM TAIFA LEO SIKU YA MATOKEO YA UCHAGUZI

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbali katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma katika Mkutano Mkuu wa Tisa ambapo leo ni siku maalum ya matokeo.


 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi akifurahia burudani inayotolewa na kikundi cha brass band cha UVCCM Zanzibar katika Chuo cha Mipango ikiwa ni siku ya pili ya uchaguzi wa UVCCM ambayo ni siku maalum kwa ajili ya matokeo ya kura zilizopigwa jana.
Viongozi mbali mbali wa CCM na UVCCM wakimsubiri mgeni rasmi ambaye ni  Makamu  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein  katika hafla ya kutangaza matokeo ya UVCCM Taifa huko Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa(kushoto) akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (kulia) na viongozi wengine wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi (kushoto) akisalimiana na Katibu wa NEC, Idara ya Organizesheni CCM taifa Pereila Ame Silima (kulia) wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma wakisubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa UVCCM Taifa.













Hakuna maoni:

Chapisha Maoni