Jumapili, 10 Desemba 2017

UVCCM TAIFA YAFANYA MKUTANO WAKE WA TISA.

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (kulia) wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM).-2017.
 Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wakiwa katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo Dodoma.



 Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Hamid Saleh Muhina(kulia aliyesisimama) akibadilishana mawazo na mjumbe wa Mkutano huo kutoka Mkoa wa Tanga.

 BAADHI ya wajumbe mbali mbali wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa wakipiga makofi na kuimba nyimbo za Chama cha Mapinduzi za kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli  katika Mkutano Mkuu huo.
 NA IS-HAKA OMAR, DODOMA.

LEO  Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) unafanya Mkutanmo Mkuu wa Tisa(9) mjini Dodoma, wakitanguliwa na falsafa yenye ujumbe unaosema “Vijana tumethubutu na tumeweza”.

Mkutano huo ni maalum kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa Umoja huo kwa ngazi ya taifa.

Mgeni rasmi katika mkutano huo ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Viongozi wengine ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndg. Abrahman Omar Kinana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdallah Juma Mabodi.

Viongozi wengine ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa pamoja na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi.

UVCCM ikiwa ni miongoni mwa jumuiya za Chama Cha Mapinduzi wanawachagua viongozi mbali mbali watakaowatumikia vijana wenzao kwa umakini na uadilifu kwa miaka mitano ijayo.

Mbali na uchaguzi huo pia mkutano huo ni sehemu muhimu ya kuwakutanisha vijana wa Tanzania nzima sehemu moja kwa lengo la kubadilishana mawazo na kupewa nasaha mbali mbali kutoka kwa viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni