NA IS-HAKA OMAR, DODOMA.
VYAMA rafiki wa Chama cha Mapinduzi, Rafiki wa Chama cha
Mapinduzi vimeutaka Umoja wa Vijana Tanzania, kuutumia wakati huu wa awamu ya
tano ya rais John Pombe Magufuli, kushirikiana na serikali yao ili kuwaletea
watanzania maendeleo yao.
Wakitoa salamu zao viongozi wa Umoja wa Vijana kutoka chama
cha Frelimo cha Msumbiji, Chama ha ZANU PF cha Zimbabwe, Chama cha EFDD cha
Burundi na Shirika la Ujerumani EFD, walisema wanaipongeza serikali ya Tanzania
kwa jitihada inazozichukua hivi sasa za kubadili maisha ya Watanzania.
Wamesema Tanzania hivi sasa imeonesha mfano mkubwa katika
dunia katika kitekeleza vyema dhamira yake ya kuwapatia maisha bora watanzania
na watakuwa tayari kuitangaza katika kiuwekezaji.
Mwakilishi kutoka Burundi, Inocent Havizirimbe, amesema nchi
yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuona wanaingia katika shughuli
za uwekezaji, ambazo zitaweza kusaidia ajira kwa vijana.
Kutokana na hilo amewaomba vijana wa Tanzania kuisaidia nchi
yao kuweza kufikia malengo yake ya mabadiliko na nchi yake itakuwa tayari
kuungana nao.
Mwakilishi
huyo, alisema tayari hivi sasa, imeshaingia mkataba na serikali ya Tanzania wa
kampuni ya Jitegemee, ikiwa ni hatua itayoweza kufanyakazi pamoja na
Watanzania.
Nae
Mwakilishi kutoka nchini Zimbabwe, amesema serikali ya nchi hiyo chini ya Rais
mpya, iko pamoja na Chama tawala cha Tanzania katika kuhakikisha wanaendeleza
umoja katika mataifa ya nchi za ukobozi.
Mwakilishi
wa Chama cha Frelimo kutoka Msumbiji, ameeleza kuwa vijana wa Tanzania wanapaswa
kuutumia vyema wakati huu kuona wanakisaidia Chama chao kwa kutambua wako
katika mabadiliko ya vita dhidi ya rushwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni