Jumamosi, 17 Februari 2018

PICHA: Watumishi wa CCM washiriki katika Mazishi ya Nd. Maulid Sleyum

Watumishi wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar leo hii wameshiriki katika Mazishi ya mtumishi mwenzao Nd. Maulid Sleyum. Maishi hayo yalifanyika huko kijijini kwao
Zingwezingwe Wilaya ya kaskazini B.

Mara tu baada ya kuwasili , Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Dk. Abdulla Juma Saadalla akisamiliana
na mmoja kati ya Ndugu wa marehemu Maulid Sleyum aliyefariki jana katika hospitali ya Global Vuga.
Miazishi hayo yalifanyikahuko Zingwezingwe wilaya ya Kaskazini B
Wanandugu, Majirani na Marafiki wakiuombea Dua mwili wa Marehemu kabla ya kuelekea Mskitini kwa
 ajili ya kusaliwa kama ilivyo taratibu ya Dini
Marafiki Ndugu na Jamaa wakiwa wamembeba mwili wa marehemu kwa ajili ya kupeleka Mskitini kama ilivyo
kawaida ya Maiti za kiisilamu hushwaliwa kwanza kabla ya kuzikwa
Dk. Mabodi, Ndugu na Jamaa wakiitikia dua  mara tu baada ya kumaliza kumsalia maiti 



Kama ilivyo kawaida kwa Binaadamu baada ya kufariki hutakiwa kuzikwa sasa hapa
 Ndugu, Jamaa na Marafiki wakiwa katika harakati za kuzika .
Tunakuomba Ya Rabi mpe makaazi mema ndugu yetu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni