KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organaizesheni Zanzibar Bakari Hamad Khamis |
KATIBU mpya wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organaizesheni Bakari Hamad Khamis ameahidi kushirikiana na viongozi na watendaji na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kupanga mikakati endelevu itakayoipatia ushindi CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Amesema hakuna Chama wala mwanasiasa yeyote wa upinzani mwenye uthubutu wa kuzuia dhamira ya Chama Cha Mapinduzi isiongoze Dola.
Msimamo huo ameutoa leo baada ya Makabidhiano ya Ofisi kutoka kwa Katibu mstaafu wa Idara hiyo Haji Mkema Haji yaliyofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Katibu huyo Bakari amefafanua kwamba atatumia uwezo aliokuwanao katika kisiasa, kiuongozi na kiutendaji kuhakikisha anasimamia na kutekeleza majukumu ya Idara hiyo yaliyotajwa katika Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2017 ibara ya 107 (1) (a),(b), (c),(d) na (e) ambayo kimsingi ni miongozo ya kiutendaji.
Akiyataja majukumu hayo kuwa ni kushughulikia masuala yote ya wanachama wa CCM, Kufuatilia vikao na Maamuzi ya Vikao vya Chama, kusimamia Jumuiya za CCM na Wazee wa Chama, Kusimamia masuala yote ya Uchaguzi wa ndani ya CCM na ule wa uwakilishi katika Vyombo vya Dola pamoja na Kusimamia Katiba, Muundo, KanuninaTaratibuza Chama na Jumuiya zake.
Kupitia hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya Ofisi, Katibu huyo mpya ametaja vipaumbele vyake kuwa atakusanya na kufanya uhakiki wa takwimu za wanachama na Wapiga kura wote ili aweze kupata takwimu sahihi zitakazokisaidia Chama Cha Mapinduzi kupata ushindi wa kihistoria katika Uchaguzi mbali mbali ujao.
“ Kwanza nawashukuru sana Wajumbe wote wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar kwa kuniamini na kunipa jukumu hili la Kiutendaji, na mimi na waahidi kuwa sitowaangusha nitakuwa kiongozi mwaminifu kwa wanachama wote na wananchi kwa ujumla.
Lakini pia na amini kwamba ili Chama Chetu kiweze kushinda bila vikwazo ni lazima tuwe na takwimu sahihi za Wanacham ana Wapiga kura wetu wote”, amesema Bakari.
Hata hivyo alikitaja kipaumbele kingine kuwa nikufanya ziara za mara kwa mara kuanzia ngazi za Mashina hadi Mikoa kwa lengo la kubaini Changamoto zinazowakabili Wana CCM na Wananchi kwa ujumla sambamba na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Pamoja na hayo ameahidi kushirikia na Watendaji mbalimbali waliostaafu katika Idara hiyo pamoja na Idara nyingine ili kupata mawazo na uzoefu wao wa kiutendaji kwa lengo la kutekeleza kazi za Chama kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza Katibu Mstaafu wa Idara hiyo, Haji Mkema Haji amewashukuru Viongozi, Watendaji na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia ngazi za Mashi na hadi Taifa waliomuunga mkono katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya Utendaji wake.
Amesema mara baada ya kumaza kipindi chake cha Uongozi ataendelea kutumia uzoefu wake kwa kuwa elimisha wanachama wa CCM ili waweze kudumu katika misingi ya uadilifu, uzalendo na kuwa makada wa kweli Chama Cha Mapinduzi.
Kada huiyo ameteuliwa jana na Wajumbe wa Kikao Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu CCM Taifa Zanzibar kilichofanyika jana Afisi Kuu CCM Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni