CHAMA Cha Mapinduzi(CCM),Zanzibar, kimetoa mkono wa rambirambi kwa familia ya mtoto aliyefariki, Tarik Abubakari,(3) baada ya nyumba kungua, Magomeni, visiwani humu.
Akitoa mkono wa pole kwa niaba ya Chama, Katibu wa Idara ya Mambo ya
Siasa, Ushirikiano wa Kimataifa,Maalim Kombo Hassan Juma , kwa familia hiyo
alisema CCM imesikitishwa sana na tukio
hilo la ajali ya moto ambalo lilitokea mnamo Februari 16, mwaka huu na
kusababisha kifo cha mtoto.
Katika maelezo yake Katibu huyo aliongeza kuwa kwa niaba ya CCM, idara
hiyo imeona ni vyema kufika kwa familia hiyo na kuungana nao ili kuwapa faraja
kutokana na tukio hilo.
"Tulipata taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari kuwa kumetokea
tukio la ajali ya moto ambalo lilisababisha kutokea kwa kifo cha mtoto wa kiume
hivyo tumekuja kutoa ubani ambao kwa namna moja ama nyingine
itasaidia,"alisema.
Kwa upande wake akitoa shukrani kwa niaba ya familia, Hamis Salum
Nassor, alishukuru kwa CCM kwa namna tukio hilo walivyolichukuliwa kwa uzito
mkubwa na namna walivyoguswa.
Alisema kitendo cha CCM kufika kuwatembelea familia hiyo ni faraja kubwa
kwao na kwamba imewapa imani ya kuwa na subira kwa wakati ambao ni mgumu.
"Tunachosema kwa niaba ya familia ni kiwa kama babu wa mtoto
aliyefariki tunawashukuru sana CCM kwa namna mlivyochukulia swala hilo uzito na
kipeumbele hivyo tunaomba mungu atupewe wepesi wake,"alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni