Alhamisi, 22 Februari 2018

UWT YASEMA MAFANIKIO YALIYOFIKIWA NI UCHAPAKAZI NA JUHUDI ZA WASTAAFU



 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Thuwayba Kisasi aklisalimiana na Akina Mama wa UWT wa Kwalamsha Jimbo la Kwahani Unguja katika mwendelezo wa ziara yake ya kuwatembelea waasisi, viongozi na watendaji wa UWT.
 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi(kushoto) akimkabidhi zawadi mwasisi wa Umoja huo Bi.Mtumwa Fikirini(kulia)  mara baada ya kumtembelea Nyumbani kwake Kwalamsha Mkoa wa Mjini Magharibi.
 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi(kushoto) akimkabidhi zawadi mwasisi wa Umoja huo Bi. Khadija Jabir(kulia) mara baada ya kumtembelea Nyumbani kwake Kariakoo Mkoa wa Mjini Magharibi.
 KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Kondo(kulia) akifuatilia matukio mbali mbali katika ziara hiyo.
 KATIBU Msaidizi UWT  Afisi Kuu Zanzibar  Ndugu Mgeni  Ottow(kushoto) pamoja na Katibu wa UWT Mkoa Mjini Asya Juma(kulia).

 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi(kushoto) akimkabidhi zawadi mwasisi wa Umoja huo Bi. Mariam Mohamed(kulia) mara baada ya kumtembelea Nyumbani kwake Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

 KATIBU wa UWT Mkoa wa Kusini Unguja Ndugu Stahamili Omar (aliyesimama ) akizungumza katika ziara hiyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi katika mwendelezo wa ziara ya kuwatembelea waasisi wa UWT.

 MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Kusini Unguja Shemsa Abdalla Ally(aliyesimama) akimkaribisha mgeni rasmi wakati wa mwendelezo wa ziara ya kumtembelea mwasisi wa UWT Bi. Mariam Mohamed(wa pili kushoto).

 KAIMU Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Kondo(aliyesimama kushoto)  akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa UWT Ndugu Thuwayba Kisasi aliyemtembelea muasisi UWT Bi.Mariam Mohamed (wa pili kulia) nyumbani kwake Tunguu.

 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Thuwayba Kisasi (kushoto) akimkabidhi zawadi Muasisi wa UWT Bi. Sihaba Farhan Ismail(kulia) katika mwendelezo wa ziara yake ya kuwatembelea Waasisi wa Umoja huo.

 VIONGO wa UWT wakitoka nyumbani kwake Bi.Sihaba Farhan Ismail hapo Kikwajuni Zanzibar.

Muasisi wa UWT Bi.Mvita Mussa Kibendera(kulia) akizungumza na  Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Thuwayba Kiasa(kushoto) wakati alipotembelea leo nyumbani kwake Michenzani Unguja.
 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi (kushoto) akimkabidhi zawadi mwasisi wa Umoja huo Bi. Mvita Mussa Kibendera(kulia) mara baada ya kumtembelea Nyumbani kwake Michenzani Mkoa wa Mjini Magharibi.

 Muasisi wa UWT Bi.Mvita pamoja na wageni kutoka ngazi ya UWT Taifa waliomtembelea wakisoma dua ya kuombea waasisi waliofariki pamoja ziara hiyo iwe ya  mafanikio.
 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi(kushoto) akimkabidhi zawadi Muasisi wa UWT Bi.Asha Simba alipotembelewa nyumbani kwake kilimani Unguja.

 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi(kushoto) akimkabidhi zawadi Muasisi wa UWT Bi.Panya Sariboko alipotembelewa nyumbani kwake kilimani Unguja.
  MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi akisaini kitabu cha wageni cha UWT Jimbo la Kwahani alipoenda kumtembelea muasisi wa UWT Bi.Mtumwa Fikirini.




 NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MAKAMU Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT),Thuwayba Kisasi, amesema maendeleo yaliyopatikana ndani ya Umoja huo yametokana na juhudi, uchapakazi na ushirikiano wa kudumu wa waasisi, viongozi na watendaji wa zamani wa Umoja huo.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizungumza katika maeneo tofauti kwenye mwendelezo wa ziara yake ya kuwatembelea viongozi na watendaji wastaafu wa Umoja huo waliowahi kufanya kazi Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, amewataka viongozi na watendaji wa sasa kutumia ushauri na maelekezo ya viongozi wa zamani kama nyenzo ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya UWT.

Ndugu Thuwayba amesema ili Umoja huo uweze kuendelea kufanya kazi zake vizuri kisiasa, kiutendaji na kiuongozi ni lazima viongozi na watendaji wa taasisi hiyo, kushirikiana na kufanya kazi kwa mujibu wa miuongozo ya kikanuni na Katiba ya CCM ya mwaka 1977 kwa lengo la kutekeleza kwa vitendo mambo mema yaliyotekelezwa na wastaafu hao.

Makamu Mwenyekiti huyo amewataja viongozi hao wa zamani kuwa ni hazina inayotakiwa kuenziwa kwani wakati wa uongozi wao wamefanya mambo yenye manufaa kwa Taifa ambayo ndio chimbuko la Chama cha Mapinduzi  kuwa imara tangu enzi za ASP.

“ Viongozi wetu wastaafu wa UWT wametulea katika misingi bora inayotuwezesha leo kuwa na uwezo wa kusimama popote kujenga hoja imara na kuwaongoza wengine bila hofu.

Lakini huu ni mwanzo tu bali tutaendelea kukutembeleeni mara kwa mara ili muweze kutuongoza sambamba na kuzifanyia kazi kwa wakati nasaha zenu.”, amesema Makamu Mwenyekiti huyo.

Nao waasisi hao wakizungumza kwa wakati tofauti wamesifu kasi ya kiutendaji ya Makamu Mwenyekiti huyo na kumuelekeza aendelee kufanya ziara za mara kwa mara kwa lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili Akina mama na wananchi wote na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Kwa upande wake Bi. Mtumwa Fikirini aliyewahi kushika nyadhifa mbali mbali za Uongozi toka enzi za ASP, amesema ili UWT iendelee kuwa imara ni lazima viongozi na watendaji wawe sehemu ya kukabili changamoto za Wanawake na wananchi kwa ujumla.

Aliwashauri Viongozi hao wa UWT kuhakikisha wanakuwa karibu na vijana wa UVCCM ili kuwafunza mambo mema ya uongozi, maadili na siasa zenye tija kwa wananchi wote, kwani vijana hao ni muhimu kuwaanda hivi sasa kwa lengo la kuwa viongozi wazuri wa baadae.

Naye Bi.Mariam Mohamed amewasisitiza UWT kuendelea na utamaduni wa Umoja na mshikamano katika maisha yao ya kila siku, huku wakikilinda na kukipigania Chama cha Mapinduzi kwa kila Uchaguzi kiendelee kuongoza nchi kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Ziara hiyo imefanyika UWT Mkoa wa  Mjini na Kusini Unguja kwa kuwatembelea viongozi hao akiwemo Bi.Sihaba Farhan Ismail, Bi, Mvita Mussa Kibendera, Bi.Asha Simba, Bi. Panya Sariboko, Bi. Mtumwa Fikirini, Bi. Khadija Jabir pamoja na Bi. Mariam Mohamed.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni