Alhamisi, 1 Februari 2018

MATUKIO KATIKA PICHA KONGAMANO LA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 41 YA KUZALIWA KWA CCM LILILOFANYIKA LEO ZANZIBAR.

 MJUMBE wa Kamati Kuu CCM Taifa Zubeir Ali Maulid akifungua Kongamano la Sherehe za maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM lililofanyika leo katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.


Baadhi ya Washiriki katika Kongamano la Sherehe za maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM lililofanyika leo katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Baadhi ya Wasjiriki wa Kongamano la Sherehe za maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM lililofanyika leo katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakiburudika na nyimbo mbali mbali za Chama Cha Mapinduzi. Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Tabia Maulid Mwita(wa pili kushoto) akiwa ni mmoja ya Maafisa wa Sekreterieti ya Uratibu wa Kongamano hilo.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Masanja Kadogosa akitoa mada ya Mchango wa CCM kuelekea Mapinduzi ya Viwanda.

 Mwanasiasa Mkongwe Visiwani Zanzibar Baraka Mohamed Shamte akitoa ufafanuzi juu ya mada ya ''Miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM kumetimiza malengo ya ASP na TANU'' katika Kongamano hilo.
Mwakilishi wa Jimbo la Shauri Moyo Unguja, Hamza Hassan Juma akichangia mada ya Mchango wa CCM kuelekea Mapinduzi ya Viwanda  katika kongamano hilo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ''Mabodi'' akizungumzia matunda ya kuungana kwa ASP na TANU na ikazaliwa CCM Mwaka 1977.WAZIRI wa Viwanda na Masoko Mhe. Amina Salum Ali akifafanua mikakati ya SMZ kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2015/2020, katika kongamano la Sherehe za maadhimisho ya Miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM.
KADA Mkongwe wa CCM  Ramadhan Abdallah Shaaban akizungumza katika kongamano hilo.
MNEC Amin Salimin akichangia mada mbali mbali zilizotolewa katika kongamano hilo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib akizungumza katika kongamano hilo kabla ya kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk. Abdulla Juma Saadalla.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharib Ayoub Mohamed Mahmoud  akiwa katika Kongamano hiloHakuna maoni:

Chapisha Maoni