Jumamosi, 3 Februari 2018

DK.MABODI ASISITIZA MIRADI YA TASAF IWANUFAISHE WALENGWA

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akizungumza na baadhi ya vikundi vilivyonufaika na mradi wa TASAF  Kaskazini Unguja.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema miongoni mwa miradi ambayo inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ni sehemu ya utekelezaji wa sera za CCM katika kuwakomboa wananchi maskini hususan kaya maskini.

Hayo aliyasem wakati akitembelea miradi mbalimbali iliyotekelezwa na mfuko huo wa TASAF upande wa Wilaya ya Kaskazini Unguja, ambapo alisema CCM itaendelea kutekeleza ahadi zake kwa vitendo ili kuhakikisha wananchi wanaondoka na katika wimbi hilo la umaskini. 

Alisema mradi huo ni moja ya mikakati ya chama katika kuinua uchumi na kipato cha mwananchi mmoja mmoja, ambapo utekelezaji wake uko katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2015/2018. 

Naibu huyo Katibu Mkuu Dk.Mabodi aliongeza kuwa mradi huo una awamu tatu ikiwemo uimarishaji wamiundo mbinu, kuwezesha makundi yasiyojiweza wakiwemo  akina mama walioko kwenye kaya maskini ili waweze kujitegemea kiuchumi na kuingia katika kundi la watu wenye kipato cha kati.

“Miradiya TASAF imeendelea kufanya vizuri kutokana na juhudiza CCM katika kuisimamia serikali itekeleze kwa wakati miradi yote ya ndani na inayotoka nje kwaajili ya ufadhili wa mipango ya maendeleo ya ndani.

Nawapongeza Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raiswa Zanzibar kwa kuratibu miradi hii mpaka ikawafikia wananchi ambao ni walengwa.”,alisema Dk.Mabodi.

Pia aliishauri Serikali kuhakikisha inaendelea kufanya tathimini na uhakiki wa kitaalamu juu ya wananchi wa naopatiwa miradi hiyo kama kweli inawanufaisha watu waliokusudiwa na sio wenye uwezo kiuchumi.

Pamoja na hayo aliwataka wananchi wa wanaonufaika na miradi hiyo kuhakikisha wanaitumia vizuri na kupata mtaji wa kuendeleza shughuli zao ili awamu zingine ziwanufashe wananchi wengine.
Mradi huo hadi sasa kwa upande wa Unguja zimetumika shilingi bilioni 12, katika utaratibu wa uhaulishaji na ajira za muda kwa fedha wanazopatiwa kaya maskini.

Aidha jumla ya miradi 190 inatarajiwa kutekelezwa kwa mwaka huu katika shehia 140, katika mwaka 2017/2018.
Naye Kaimu Sheha wa Shehia ya Donge Mnyimbi ambaye ni Sheha wa Mkataleni Ndugu Sharif Ali ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapelekea mradi huo uliosaidia kubadilisha maisha ya wananchi wengi wanaoishi katika kaya maskini na wamepata mitaji ya kujimudu kimaisha.

Ameeleza kuwa changamoto zinazovikabili baadhi ya vikundi vya ujasiriamali kwa Akina Mama wa Shehia hiyo ni upungufu wa mitaji pamoja na kukosa visima vya uhakika kwa upande wa Akina mama wanaojishughulisha na upandaji wa miti katika vitaru.

Katika ziara hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi alitembelea vikundi mbalimbali vya Ujasiriamali vya Akina Mama wa Shehia za Donge Mnyimbi, Kijimbwen, Muwange, Chuini, Bumbwi sudi pamoja na Kizimbani.
                                                    Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni