Ijumaa, 9 Februari 2018

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA DK.MABODI PEMBA

 NAIBU katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk Abdulla Juma Mabodi, akiangalia moja ya ramani za ujenzi wa mradi mkubwa wa uwekezaji wa Chama Cha mapiduzi Wilaya ya Micheweni, wakati wa ziara yake ya Kicha kwa Wilaya hiyo

 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk Abdulla Juma Mabodi, akisalimiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni, wakati alipowasili Chimba kuzungumza na Viongozi na wanachama wa CCM Tawi la Chimba, wakati wa ziara yake ya kuzungumza na wanachama hao.

 BAADHI ya wanachama na viongozi wa CCM Wilaya ya Micheweni, wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdulla Juma Mabodi, wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na wanachama wa CCM Tawi la Chimba Jimbo la Tumbe Wilaya ya Micheweni.

 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar,  Dk Abdulla Juma Mabodi, akizungumza na Viongozi na Wanachama wa Tawi la CCM chimba Wilaya ya Micheweni, wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Micheweni.
 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi , akifurahia jambo na Mwasisi wa CCM Wilaya ya Micheweni, Bi.Mrashi Seif wakati alipotembelewa nyumbani kwake Shehia ya Sizini Wilaya ya Micheweni.

 NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Mhe:Dk Abdalla Juma Mabodi, akikagua ujenzi wa nyumba ya bimrashi Seif inayojengwa na CCM Wilaya ya Micheweni, huku akiahidi CCM Afisi kuu ya CCM  Zanzibar ikiahidi kumjengea  Choo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni