Jumatatu, 5 Februari 2018

BI. SIHABA ISMAIL FARHAN-AICHAMBUA MIAKA 41 YA CCM

 MUASISI wa ASP Bi.Sihaba Ismail Farhan.

MUASISI wa Afro-Shiraz Party (ASP) Bi. Sihaba Ismail Farhan amesema tunu ya urithi wa Uongozi bora na Demokrasi vilivyoasisiwa na Viongozi wa ASP na TANU leo vinatekelezwa kwa vitendo na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo ameitoa leo katika Mahojiano Maalum na Kitengo Cha Habari Cha Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, amesema miongoni mwa tunu hizo zilizoenziwa ndani ya kipindi cha miaka 41 ya CCM ni pamoja na uimarishaji wa dhana ya utawala bora, Sekta za Elimu, Afya, Uvuvi, Kilimo, Miundombinu katika Sekta za Anga, Nchi kavu na Baharini.

Amesema maendeleo yaliyofikiwa katika Nyanja hizo ni juhudi za kiutendaji zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Saba chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohamed Shein.

Hata hivyo Bi.Sihaba ameongeza kuwa Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua kwa kasi kutokana na Uelezi na ustadi wa CCM katika usimamizi mzuri wa Sera zake kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama.

Aidha Muasisi huyo ambaye pia ni Mtaalamu wa masuala ya utetezi wa Haki za Wanawake nchini, alisema ndani ya miaka 41 yakuzaliwa kwa CCM, Chama kimeruhusu mfumo huru wa ushindani wa kisiasa unaowawezesha wanawake wengi kupata nafasi za ngazi za juu katika Vyombo vya kufanya maamuzi.

Amewapongeza Marais wote ambao ni Raiswa Zanzibar  Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa kulinda Muungano waasili wa Serikali mbili ambao ni moja kati ya urithi wa ASP na TANU.

Pamoja na hayo ameiponge za Serikali ya Awamuya Saba yaMapinduziya Zanzibar ChiniyaUongoziwa Dk. Shein kwa kujali maslahi ya makund imbalimbali wakiwemo Watu wenye ulemavu, Watoto na Wazee.

“Dk. Shein ameanzisha pencheni ya Wazee bila ubaguzi kwa sasa kjla mwezi tunapata shilingi 20,000 Mwenyezi Mungu amjalie mema kwani maamuzi kitendo hiki kina ni kumbusha Enzi za Marehemu Mzee Abeid Karume jinsi alivyokuwa akiwajali Wazee”, anaeleza

Mapema akitoa historia ya CCM alisema mnamo Februari 5, 1977 bendera za ASP na TANU zilishushwa na kupandishwa pendera moja ya CCM, ambapo wananchi wengi waliudhuria hafla hiyo.

Amesema vyama vya Upinzani vinatakiwa kujitathini kwa kina juu ya uwepo wao katika Mfumowa Vyama vingi kama wakidhi matakwa ya uwepo wa mfumo huo huku wakiiga mambo mema yaliyofanywa na yaliyotekelezwa na CCM.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni