Jumatano, 21 Februari 2018

CHAMA CHA MAPINDUZI CHALAANI VIKALI VITENDO VYA UZALILISHAJI




TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. 

Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshituko mkubwa sana juu ya kuendelea kwa wimbi kubwa la unyanyasaji wa kijinsia linaloendelea kwa kasi katika jamii yetu kila siku mambo yanazidi kupamba moto katika jambo hili limetushitua sana na kutufanya kutokuwa na furaha katika shughuli zetu za kila siku juu ya mwendo wa matukio haya. Kwanza kabisa tunatoa pole kwa wale ambao wameguswa na matukio haya kwa namna yeyote ile tunawaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu kwao kama familia lakini tunawambia kuwa tupo pamoja katika maumivu haya ambayo hakika hayavumiliki kabisa poleni sana tuna amini kuwa kwa pamoja tutashinda dhidi ya uovu huu kwa pamoja .

Tunaomba wale wote ambao wameguswa na matukio haya na wanafahamu matukio haya tunaomba kuyaripoti katika vituo vya polisi na Vyombo vya Dola kwani kufuatia mabadiliko makubwa ya sheria hivi karibuni ya sheria namba mbili ya 2018 kwamba kasi ya utekelezaji wa ilani itakuwa kubwa zaidi na kupelekea kupata haki kwa haraka bila ya uonevu. Chama Mha Mapinduzi tunaviomba Vyombo vya Dola kufanya operation maalumu juu ya matukio haya ambayo kila siku hapa zanzibar yamekuwa yakichukua kasi kubwa sana tunafahamu kuwa kwa mkurugezi wa mashataka yapo mashataka zaidi ya 150 ya watu mbali mbali lakini bado hayajapelekwa mahakamani kwa sababu mbambali tunawaomba wajitahidi kukamailisha uchunguzi na taratibu kwa haraka ili jamii iweze kuona namna ya matukio haya yanavyoweza kukomeshwa. 

Chama cha Mapinduzi ambao ndio wasimamizi wa ilani ya uchaguzi ya CCM tunaona kwamba lazima tuongeze kasi ya usimamizi wetu kwa kuwakumbusha kuwa Chama pamoja na jamii yetu inakwerwa na matukio haya hivyo tunaomba wasimamizi wa sheria kuongeza kasi juu ya matukio haya. Mwisho Chama Cha Mapinduzi kipo nanyi pamoja katika kuhakikisha kuwa ustawi wa watu na maisha yao ndio jambo kubwa la muhimu hivyo tutaakikisha sheria kali zinachukuliwa kwa kupitia vyombo vya dola huu ndio wajibu wetu Ahsateni sana,

 “KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI”





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni