KATIBU wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi.Catherine Peter Nao (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Iland Media Group Bw.Fauz Abdul Razaki (kushoto). |
KATIBU wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi.Catherine Peter Nao, akiwa katika studio za Zenj Fm. |
Mkurugenzi Iland Media Group Bw.Fauz Abdul Razak (kushoto), akitoa ufafanuzi wa vifaa vya kurushia matangazo ya TV katika Chumba maalum cha kuzalisha vipindi. |
Katibu wa Idara ya NEC, Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi.Catherine Peter Nao akiwa katika Studio za Coconut Fm Radio iliyopo Migombani Mnara wa Mbao Zanzibar. |
KATIBU msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Daud Ismail Juma akitambulisha maafisa mbali mbali wa CCM waliofustana na Mkuu wa Idara hiyo. |
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi. Catherine Peter Nao akiwa katika studio za Bomba Fm Radio. |
Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi. Catherine Peter Nao (kushoto) akizungumza na Bw. Aziz(kulia) Mkuu wa udhibiti wa fedha wa Bomba FM Radio. |
Katibu wa Kamati
Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Bi. Catherine Peter Nao katika mwendelezo wa
ziara, akiwa katika Chumba Cha kuzalisha Vipindi vya Iland TV.
|
MKUU wa Vipindi Tifu TV Bw. Mwanjie Saleh Mgeni (kulia wa mwanzo) akitoa ufafanuzi juu wa chumba cha matangazo cha Tifu TV, Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi akifuatilia kwa makini maelezo hayo. |
Chumba cha kurushia matangazo cha Tifu TV. |
Meneja
Mkuu wa Tifu TV Bw.Abdalla Kesi Shaaban(kulia)
akizungumza na Katibu wa Kamati Maalum
ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar
Bi. Catherine Peter Nao akizungumza na viongozi na watendaji wa Zenj Fm
Radio katika ziara yake kwenye vyombo vya Habari Zanzibar.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao amesema Vyombo vya Habari ni taasisi muhimu zinazotakiwa kuwa mstari wa mbele kukemea na kuibua vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto ili wahalifu wa matukio hayo waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Kauli
hiyo ameitoa katika mwendelezo wa ziara yake kwenye Vyombo vya Habari nchini,
amesema taasisi hizo zenye dhamana ya kuelimisha,kuburudisha,kukosoa na kushauri
zina jukumu kubwa la kueleza kwa upana athari mbaya zinazotokana na vitendo
hivyo.
Alisema
Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuishauri serikali na wadau mbali mbali wa haki
za binadamu kutekeleza wajibu wao wa kuvisimamia vyombo vya kisheria
kuharakisha uendeshaji wa kesi hizo na kutoa hukumu kali kwa watu wanaotiwa
hatia kwa makosa hayo.
Pia,
alilitaka Jeshi la Polisi nchini kuondokana na mfumo duni wa upelelezi juu ya
kesi za udhalilishaji badala yake waongeze kasi na kutumia weledi na uaminifu
kama kanuni na miongozo ya jeshi hilo inavyowaelekeza.
Katibu huyo alisema
tayari serikali imeanza kuchukua hatua ikiwemo Baraza la wawakilishi kupitisha
mswaada wa sheria mpya ya mwaka 2018, inafuta sheria ya adhabu kwa makosa ya
jinai ya mwaka 2004, hivyo baada ya Rais wa Zanzibar kuitia saini na kuwa
sheria kamili kinachobaki ni wananchi na wadau wengine kuunga mkono juhudi
hizo.
“ CCM ni
taasisi inayojali misingi ya haki za binadamu na utu kwa watu wote bila kujali
tofauti za kisiasa, hivyo hawezi kubaki kimya huku nchi yetu inaendelea
kuangamia kwa vitendo viovu vya ubakaji kila sehemu, ni muhimu kila mtu
kupambana kwa nafasi yake ili tuondoshe janga hili.
Lakini pia
taasisi zinazosimamia masuala ya utekelezaji wa Kisheria sasa tunawambia huu
ndio muda wa kujitathimini na kufanya kazi vinginevyo Chama Cha Mapinduzi
kitachukua hatua kali za kimaadili kwa baadhi ya viongozi wakuu wa Taasisi hizo
ambao hawatekelezi wajibu wao kiutendaji”, alisema Bi,Catherine.
Hata hivyo
alieleza kuwa Zanzibar haikuwa na utamaduni wa kesi za aina hiyo lakini vitendo
hivyo vimeongezeka kutokana na utandawazi unaopelekea baadhi ya wananchi kuacha
utamaduni wa asili na kuiga masuala ya kigeni.
Akizungumzia
mchango wa vyombo vya Habari katika ukuaji wa Demokrasia, Catherine amesema
taasisi hizo za kihabari zimekuwa mstari wa mbele kuandika na kuripoti vipindi,
makala na habari mbali mbali za kisiasa zinazochangia ukuaji wa kidemokrasia
kwa wananchi.
Alisema
Vyombo vya habari sio tu kutangaza habari za kisiasa bali hata katika ukuaji wa kiuchumi
wa Zanzibar taasisi hizo zimechangia kutangaza
fursa za nchi katika anga za
kimataifa hasa utaliii na zao la karafuu na kusaidia ukuaji wa pato la taifa
unaotokana na upatikanaji wa fedha za kigeni.
Pamoja na
hayo alisema lengo la ziara hiyo ni kujitambulisha,kubadilishana mawazo,
kujenga mahusiano kwa vyombo hivyo
ambavyo ni wadau wakubwa wa CCM katika masuala ya kueneza Itikadi na Habari za
Chama kwa wananchi.
Ameahidi
kuendelea kufanya kazi na ukaribu na vyombo vya Habari mbali mbali na
kuvishauri vielekeze nguvu zake sehemu za kijamii hasa za vijijini kuibua kero
zinazowakabili wananchi ili taasisi husika zitafute ufumbuzi wa kudumu.
Naye Meneja wa Radio ya Zenj Fm, Winifrida Mayao
amekipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa busara zake za kuendeleza mahusiano ya
kiutendaji na Kituo hicho.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Iland Media Group, Hatwab Mbarouk Khamis ameeleza kuwa ziara hiyo
imefungua milango ya kiutendaji baina ya Kituo Chake na CCM.
Akizungumza
Muhariri Mkuu Mtendaji wa Bomba Fm Radio, Mwinyi Sadala amesema Kituo hicho
kimekuwa ni mdau mkubwa wa kuripoti na kuandika habari za kisiasa, kijamii na
kiuchumi zinazohamasisha dhana ya Utawala bora, Demokrasia, uhuru wa kutoa na
kupokea maoni kwa wananchi.
Hata hivyo Sadala alikishauri Chama hicho
kuwakumbusha baadhi ya Wabunge, wawakilishi,Madiwani na viongozi wengine wa
Serikali ambao bado hawajatekeleza ahadi
walizotoa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, kutumia wakati huu kutekeleza ahadi
hizo kwa lengo la kurejesha matumaini ya jamii.
Ziara hiyo
imeendelea katika Vyombo vya Habari mbali mbali ikiwemo Zenj Fm, Coconut Fm,
Iland TV, Bomba Fm na Tifu TV.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni